Aneth Msuya enzi za Uhai wake.
Mtumishi wa Wizara ya Fedha, Aneth Msuya (30) ambaye ni mdogo wa Bilionea
Erasto Msuya aliyeuawa kwa kupigwa risasi 22 KIA, ameuawa kwa kuchinjwa
nyumbani kwake eneo la Kigamboni jijini Dar Es Salaam.
Mmoja wa ndugu wa familia hiyo, Shujaa Khamis, jana alithibitisha kuuawa
kwa Aneth, lakini alikataa kuingia kwa undani.
“Ni kweli wamemchinja usiku wa kuamkia leo (jana) na hapa nipo kwenye
msiba hapa nyumbani (Mererani) kwa baba. Tumeambiwa wamechukua Tv tu,”
alisema.
Hata hivyo, Khamis alikataa kueleza lolote kama wana mashaka na mauaji hayo
zaidi ya kuliomba Jeshi la Polisi nchini, kuchunguza kiini cha mauaji hayo na
kuwasaka waliohusika.
Habari nyingine kutoka Wizara ya Fedha, ziliwakariri baadhi ya watumishi
wakisema wamepata taarifa za msiba huo, lakini hawajapewa taarifa rasmi.
“Tuna taarifa tunazisikia sikia kuwa ameauawa, lakini jana (juzi) tulikuwa naye
kazini ila leo (jana) ndiyo tunasikia amechinjwa na watu wasiojulikana.
Imetusikitisha sana,” alisema mmoja wa watumishi hao ambaye hakutaja jina
kwa kuwa si msemaji.
Kamanda wa mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Andrew Satta alipofutwa jana
kuthibitisha taarifa za mauaji hayo alisema yuko kwenye kikao.