BREAKING NEWS

Friday, May 6, 2016

MBUNGE ROSE TWELVE KUWANUFAISHA WANAWAKE WA MKOANI IRINGA

 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Rose Twelve akifurahi jambo na wakinamama wenye ulemavu.

 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Rose Twelve akizungumza na wanawake wa chama cha mapinduzi ccm mkoani iringa.


na fredy mgunda,iringa

Wananchi mkoani iringa wanatarajia kunufaika na muungano wa wabunge watatu vijana wa viti maalu kwa lengo kubadilishana uzoefu wa kuwaletea maendeleo wanawake wa mkoa huu.

Akizungumza na blog hii Mbunge wa viti maalum mkoa wa Rose Twelve alisema wameamua kuungana ili kubadilisha mfumo wa utawala na kuondoa ufanyaji wa kazi kwa mazoea sambamba na kuwasaidia wananchi wanaowatumikia.

“Unajua kuwa changamoto na matatizo ya wanawake kwa asilimia kubwa zinafanana hivyo najifunza kwa wenzangu wanatatuaje changamoto hizo ili na mimi niweze kutatua matatizo ya wanawake wa mkoani iringa na waendelee kufanya maendeleo huku wakiwa hawana changamoto nyingi”alisema Rose

Aidha rose aliongeza kwa kusema kuwa kiongozi bora ni Yule aliyetari kujifunza ili aweze kupata ujuzi wa kuwasaidia wananchi kwa kuwapa mbinu wananchi za kuwaletea maendeleo.

Rose alisema amejipanga kuwekeza kwenye elimu ili kuwapa wanawake fursa ya kuwapa ya kuwawezesha kunufaika na mfuko wa mbunge anaotarajia kuuanzisha.

“Nitatoa milioni hamsini kila mwaka kwa umoja wa wanawake wa ccm UWT mkoani hivyo lazima nitafute njia mbadala ya kuwapa elimu ya kuzitumia hizo pesa ili ziwanufaishe kwa kuwaletea maendeleo”.alisema Rose

Lakini Rose alisema kuwa atataufa wataalamu wa mafunzo mbalimbali ili wanawake wa mkoa wa iringa wapate elimu ya ujasiliamali na kuokoa pesa ambazo zimekuwa zikipotea.

Nitatafuta wadau mbalimbali wachangie mfuko wangu wa mbunge kwa lengo la kuwasaidia wanawake ambao hawana mitaji ya kujiendesha maisha yao.alisema Rose

Amemalizia kwa kuwataka wakazi wa Iringa kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo binafsi na taifa kwa ujumla.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates