Mbunge wa jimbo
la Arumeru magharibi Gibson Olemeiseyeki akipata maelekezo ya huduma
zinazotolewa na kampuni ya utalii OSUPUKO nature Paradise(picha na maktaba)
Na Woinde Shizza, Arusha
SEREKALI Imetakiwa kuajiri maafisa uhamiaji ambao wanayo
elimu ya uongozi wa Utalii ili kuweza kuwa pokea wageni wanatoka nje ya
nchi vizuri kulingana na taaluma.
Hayo yamebainishwa na mbunge wa jambo la Arumeru magharibi
Olemeiseyeki Gibson Blasius wakati jana wakati alipokutana akiongea na waandishi
wa habari kuhusiana na nini kifanyike ili wageni wengi wa tembelee nchi
yetu kuangalia vivutio vilivyopo.
Alisema kuwa serekali inatakiwa kuajiri maafisa uhamiaji
haswa wanaokaa katika viwanja vya ndege wenye elimu ya utalii ili
kuweza kuwa pokea wageni wanaoingia Hapa nchini kwa kwa ukarimu na
kwakufuata taaluma ya utalii.
"unajua maafisa uhamiaji waliopo katika viwanja vyetu vya
ndege baadhi awana taaluma Nzuri kwani Unakuta afisa uhamiaji anampokea
mgeni kama mpwa au mualifu haliinayofanya mgeni ajisikie Vibaya mno hali
inayofanya akarudi kwa o akayangaze nchi yetu Vibaya" Alisema
Olemeseyeki
Aidha Alibainisha kuwa mbali na hivyo pia serekali
inatakiwa kutoa maelezo ya vitu ambavyo mgeni anatakiwa a fanye kabla ya
kufika Hapa nchini ili kupunguza ukumbufu ambao Unaweza kujitokeza.
"tukiangalia mfano hii sindano ya yellow fiva Unakuta
mzungu kaja kaanza kunywa vidonge vya kuzuia malaria miezi mitatu nyuma
kabla ajaja sasa anafika apa analazimishwa kuchomwa sindano kitu ambacho
sio aki na sasavunakuta apobakilazimishwa ndio Unakuta inamlazimisha
atoe rushwa ili apite ili mraw di tu asipigwe iyosindano"alisema
Olemeseyeki
Alitaka serekali kuzisafisha viwanja vyote Vya ndege kwa
kuajiri watu wenye elimu na watakao pokea wageni vizuri tangu anaposhuka
kwenye aridhi ya tanzania na kubainisha kuwa ukimpokea mgeni vyema basi
pale Atakapoondoka Hapa chini ataenda kutangaza nchi yetu na vivutio
vyema hali ambayo itasaidia kupata watalii wengi wanaokuja kuangalia
vivutio vilivyopo Hapa nchini.
Aidha Alizitaka Mamlaka husika ikiwemo Hifadhi za Taifa
(TANAPA), pamoja Hifadhi ya Taifa Ngorongoro kuboresha miundombinu
Ikiwemo vibanda vya kulia chakula mgeni akiwa ifadhini pamoja na kuweka
madawati maalumu ambayo atupeleke ma tatizo au Shida ambayo utamkuta
pindi anapokuwa Hifadhi na kujibiwa kwa haraka na wakati.