Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (kulia) akisalimiana na kumkaribisha ofisini kwake Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya, Luana Reale (katikati) walipowasili jijini Mwanza kabla ya ziara ya kukagua miradi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa pamoja na Umoja wa Ulaya.
MRATIBU Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Alvaro Rodriguez pamoja na Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya, Luana Reale, wamesema wameridhishwa na miradi inayofadhili maeneo kadhaa jijini Mwanza.
Wakizungumza baada ya kutembelea Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Mwauwasa), Hospitali ya Rufaa Bugando (BMC), Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) na Radio ya Kijamii (Saut), walisema utekelezaji wa miradi hiyo imewatia hamasa kubwa.
Awali akizungumza katika ofisi za Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Mwauwasa), Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka hiyo, Anthony Sanga, alisema mradi unaoendelea sasa wa kusambaza maji safi utakapokamilika utaweza kuwafikia wakazi 54,000 badala ya 23,000 wa sasa.
Sanga alisema mradi huo utakapokamilika Mei mwaka huu, utawafikia wakazi kwa asilimia 90 badala ya 68 za sasa.
“Mradi ukishakamilika utafanikisha makusanyo ya Sh. Bilioni 1.4 kwa mwezi badala ya kukusanya Sh. milioni 316 za sasa kwa mwezi, ukiwa na matanki ya ujazo wa lita 33,400,” alisema Sanga.
Akizungumzia hilo, Rodriguez alisema baada ya kushuhudia miradi hiyo ukiwamo wa maji taka chini ya ufadhili wa EU, amefurahishwa na hali ya miradi hiyo.
“Timu yetu imetembelea Mwauwasa na kushuhudia miradi hiyo inayofadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya kwa ajili ya huduma ya maji kwa wananchi, pia tumeenda kuangalia chanzo cha maji na yanapowekwa maji taka,” alisema Rodriguez.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Bugando, Prof. Kien Mteta, alishukuru UN na EU kwa miradi hiyo na kuja kushuhudia ufadhili wao.
“Ufadhili umelenga katika mambo matatu, moja kwenye maabara ambako vilinunuliwa vifaa vya mbalimbali vikiwamo vya kutambua kansa, pili vifaa vya mionzi kwa ajili kutambua vyanzo vya magonjwa,” alisema Prof. Mteta.
Aidha, alisema pia wafadhili hao walitembelea kitengo cha kutoa matibabu ya mionzi ya kansa, ambacho kinawafunza baadhi ya watumishi wake na upatikanaji wa mashine.
Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya, Luana Reale (katikati) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella mara baada ya kuwasili ofisini kwake mwishoni mwa wiki.
Hospitali ya Bungando yenye uwezo wa vitanda 950 iliyoanzishwa mwaka 1972 ni miongoni mwa hospitali nne kubwa nchini ambazo hutoa tiba maalumu ikihudumia watu milioni 16 katika mikoa minane ya kanda ya ziwa.
Hospitali hii inatoa tiba ya ugonjwa wa saratani kwa mifumo miwili. Moja kwa kutumia onkolojia au patholojia na tiba kwa kutumia mionzi.
Toka mwaka 2000 hospitali ya Bugando imekuwa ikifanyakazi kwa karibu na kampuni ya kitaliano ya TISSON ASSOCIATION ili kuboresha huduma zake patholiojia na pia kuanza kutibu kansa mwaka 2009.
Wataliano wamewezesha kufundishwa kwa wataalamu wa patholojia na onkolojia ya tiba, vifaa tiba, dawa na kuwezesha ziara za za kifundi za watu wa patholojia na utafiti.
Uangalizi wa wagonjwa wa kansa na matibabu yao ulianza mwaka 2009 na kuelezwa kuwa kwa mwaka wagonjwa 3500 wa kansa huangaliwa.
Huduma ya uangalizi ni pamoja na kufanya utambuzi, upasuaji na utoaji wa tiba ya kemo.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akitoa utambulisho wa ujumbe alioambatana nao kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.
Hata hivyo wagonjwa wanaohitaji huduma ya mionzi hukatiwa rufaa hospitali ya kansa ya Ocean (ORCI).
Kutokana na kuzidiwa kwa hospitali ya Ocean Road katika tiba ya mionzi, serikali iliamua kutanua huduma zake na kuzifikisha Bugando.
Ili kuwezesha haja ya serikali taasisi ya nguvu za atomiki duniani na ile ya hapa nchini kupitia mpango wa ushirikiano wa kiufundi walianzisha miradi kadha yenye lengo la kuwezesha huduma yenye tija kwa wagonjwa wa kansa.
Mashirika ya Umoja wa Mataifa ambayo yanachangia miradi hiyo imekuwa ikisaidia serikali ya Tanzania kuwezesha tiba ya mionzi katika hospitali ya Bugando.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akiwa kwenye mazungumzo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya, Luana Reale katika ziara maalum ya kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na UN pamoja na EU jijini humo.
Kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza CP. Clodwig Mtweve, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella pamoja na Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya, Luana Reale wakiwa wameshilikilia kuhamasisha utekelezaji wa malengo mapya ya maendeleo endelevu (SDGs) ambayo yamewafikia wakazi wa jiji la Mwanza.
Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya, Luana Reale akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Mwauwasa) mara baada ya kuwasili katika ofisi hizo jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Mwauwasa), Mhandisi Anthony Sanga, akitoa 'power point presentation' ya maendeleo ya mradi wa maji unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya jijini Mwanza kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya, Luana Reale aliyeambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Mwauwasa), Mhandisi Anthony Sanga akitoa maelezo ya mradi kwa ugeni ulioambata na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.
Maji yakiwa kwenye hatua ya kutakatishwa ili yawe salama kwa watumiaji.
Mhandisi wa ubora wa maji Mwauwasa, Godadi Mgwatu akitoa maelezo kwa mgeni ugeni huo ulioambatana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella kukagua mradi wa maji wa Mwauwasa jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Mwauwasa), Mhandisi Anthony Sanga akitoa maelezo kwa ugeni huo ya namna ya maji yanavyochujwa na kusafisha kwa kutumia mtambo maalum uliopo mbele yao. (Picha zaidi za ziara hii Bofya hapa)