MWIGULU ATUMBUA MAJIBU JIMBONI KWAKE.


WAZIRI wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Bw. Mwigulu Nchemba amejitolea kulipia
kiasi cha Tsh milioni 2 kwa kusaidia matengenezo ya mashine ya maji huku
akitumbua majipu kwa kuwasimamisha kazi viongozi 15 wa bodi ya maji ya
kijiji cha Mingela jimboni kwake Iramba wilaya ya Iramba mkoani Singida baada
ya bodi hiyo kufanya ufisadi wa milioni 9 za mradi wa maji wa kijiji hicho.

Viongozi hao ambao ni pamoja na Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Mingela,
Mwenyekiti, Katibu, Mhasibu na wajumbe 12 ambao walikuwa wakiunda bodi
hiyo ya maji waliwasimamishwa baada ya kutafuna pesa hizo za mradi wa maji
na kushindwa kulipia milioni 2 kwa ajili ya matengenezo ya mashine
iliyoharibika .

Nchemba ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Iramba alifikia uamuzi huo wa
kuivunja bodi hiyo ya maji kijijini hapo jana baada ya wananchi wa kijiji hicho
kulalamika katika mkutano wake wa hadhara kwa ajili ya kuwashukuru kwa
kumchagua na kuanza kutimiza sehemu ya ahadi zake, kuwa hawana huduma
ya maji safi baada kukosa Tsh milioni 2 za kutengeneza mashine ya maji
iliyoharibika kwa muda sasa.

Kutokana na kilio hicho cha wananchi Nchemba alilazimika kumwita jukwaani
Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Bw Said Mussa na bodi yake ili kueleza mapato
na matumizi ya mradi huo wa maji yapo kiasi gani na yapo wapi, swali
lililopelekea viongozi hao kujichanganya kujibu kuwa ni kweli makusanyo ya
mradi huo wa maji ni zaidi ya Tsh milioni 9.4 ila benki zipo kiasi cha Tsh
400,000 na pesa nyingine zimetumika kukarabati mashine hiyo iliyokuwa ikihitaji
kutengenezwa kwa Tsh milioni 2 .

Mganganyiko huu ulimlazimu waziri huyo kuivunja bodi hiyo ya maji na
kumwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Clement Berege
kupeleka wakaguzi wa ndani mara moja katika kijiji hicho ili kukagua mapato na
matumizi pamoja na kuwachukulia hatua wahusika wote wa ufisadi huo wa
pesa za makusanyo ya maji.

Alisema kuwa ni ufisadi mkubwa ambao umefanywa na viongozi hao wa bodi ya
maji katika kijiji hicho kwa kutafuna pesa zote pasipo matengenezo ya mashine
ya maradi huo wa maji.
“Yaani ni ufisadi mtupu ambao sikubaliani nao hata kidogo mashine ya
kutengenezwa milioni 2 imetengenezwa kwa milioni 9 na bado haifanyi kazi
…..naomba wote mliohusika na ufisadi huu kuanzia leo mkae pembeni na
wakabidhiwe ofisi watu wengine ……pia mkurugenzi kuanzia sasa vitabu vyote
vya makusanyo ya mapato vithibitiwe ili kuepusha kupoteza ushahidi ”
Hata hivyo aliuagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kutuma
wakaguzi wa ndani katika vijiji vyote vya Halmashauri hiyo ili kufanya ukaguzi
wa mapato na matumizi kwenye vijiji vyote.

Alisema yawezekana viongozi wa vijiji wamekuwa wakitumia vibaya makusanyo
ya pesa za wananchi bila kufuata utaratibu wa kusoma mapato na matumizi
kwa kila baada ya miezi mitatu kwa mujibu wa taratibu.
Katika hatua nyingine, Bw Nchemba aliutaka uongozi wa serikali za vijiji katika
wilaya hiyo ya Iramba kuacha kuendelea kuwatoza wananchi ushuru kandamizi
wa biashara ndogo ndogo hasa zile zilizopigwa marufuku wakati wa ugonjwa
wa kipindupindu kwa kutoza ushuru wa Tsh 10,000 kwa biashara ambayo
mwananchi akiuza yote faida yake anaambulia Tsh 5000 hivyo alishauri uongozi
wa Halmashauri kushusha ushuru huo ambao ulikuwa maalum kwa
mapambano ya ugonjwa wa kipindupindu na kuwatoza ushuru wa Tsh 3500
kwa wananchi wanaojishughulisha kufanyabiashara ndogo ndogo ikiwemo ya
upikaji pombe kwa ajili ya kuendesha maisha yao.

Pia alitaka wananchi kuendelea kudumisha usafi katika biashara zao ili
kuondokana na ugonjwa wa kipindupindu, kwa wananchi ambao walipatwa na
maafa wakati wa mvua kubwa zilizonyesha mwaka huu, alisema kuwa
wataalam wa maafa kutoka ofisi ya waziri mkuu watafika kufanya tathimini ili
kuwasaidia wananchi hao.

Akijibu tuhuma hizo mbele ya Waziri Nchemba, Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha
Mingela, Bw Said Mussa alisema kuwa ni kweli walikusanya milioni 9.4 za
mradi huo wa maji na fundi kutoka mjini Iramba anahitaji milioni 2 kwa ajili ya
kutengeneza mashine hiyo ila kiasi cha pesa kilichopo benki ni Tsh 400,000
pekee hivyo hawana uwezo wa kulipia gharama za fundi.

Alisema kuwa kwa upande wake hajui mhusika halisi wa ufisadi huo lakini kwa
kuwa waziri amesimamishwa kazi wote basi itasaidia kumpata mhusika



Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post