Mfanyabiashara
maarufu jijini hapa Anset Anselim
Mashallo (34) mkazi wa Unga Limited ameuwawa na mfanyakazi wake kwa kuchomwa kisu mgongoni wakati akidai kodi ya pango ya kiasi cha shilingi laki moja .
Akiongea na
waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo alisema
kuwa tukio hilo lilitokea May 19 majira
ya saa 21:15 usiku katika maeneo ya Unga limited wilayani Arusha mjini.
Kamanda
alimtaja mtuhumiwa wa mauaji hayo ni Prosper Adeline (47)mkazi wa Unga Limited
ambaye alikuwa akifanyakazi ya kuchoma nyama katika bar ya marehemu ijulikanayo
kwa jina The Place bar iliopo jirani na
kituo cha polisi ungalimited.
Alisema kuwa
mtuhumiwa wa tukio hili alikuwa na ugomvi na marehemu kwani marehemu alikuwa akimdai mtuhumiwa hela
ya pango la jiko lilikuwa ndani ya bar
hiyo ambapo alikuwa akimdai kodi ya miezi miwili.
Mkumbo
alisema kuwa hadi sasa matuhumiwa anashililiwa na jeshi la polisi kwa mahojiano
zaidi na pindi upelelezi utakapo
kamilika atafikishwa mahakamani ,na mwili wa marehemu umeifadhiwa katika
hospitali ya mkoa wa Mounti Meru .