Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Jeshi la Polisi Zanzibar limesema haliogopi kumhoji au limeshindwa
kukamkata Katibu Mkuu wa Chama Cha a2ananchi (CUF ) Maalim seif sharif
Hamad na kwanba limeahirisha tubkufanya hivyo jana ila dhamira bado iko
pale pale ya kumhoji na kumtaka atoe maelezo husika.
Aidha jeshi hilo limesisitiza kuwa linaweza kukamata kiongozi yeyote wa
kisiasa wmbaye hana kinga za kisheria kwa ajili ya mahojiano,kumtaka
atoe maelezo au ufafanuzi kuhusiana na masuala kadhaa yanayotia shaka .
Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya jinai zanzibar kamanda Salum Msangi
amethibitisha hayo jana baada ya jeshi hilo kuahirisha kufanya naye
mahojiano hadi itakaoopanga tena haraka toka sasa.
Kamanda Msangi elisema wanaofikiri kuwa polisi wameshindwa au
wanakuogopa kumhoji kiongozi hiyo hawana hoja ya msingi huku akisema
kuwa kutokana na miingiliano ya kimajukumu ndiko kulikofanya mahojiano
hayo yaaihirishwe.
"Tumeahirisha kumhoji kutokana na muoingiliqno ya majukumu yetu ya
kipolisi na si kumhofia su kumuogopa, tukitaka kumhoji jumanne akaonba
ahijiwe ijumaa (jana)ambapo nasi kutokana na sababu za kiutendaji
tumeoanga kuwita wakati mwingine "alisema .
Aidha Naibu huyo Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai alisema si muda mrefu
toka sasa jeshi hilo kutamwita kiongozi huyo wa upinzani ili kumhoji
kutokana na masuala kadhaa ambayo bado yako kwenye mabano.
Alipiulizwa kutikana na kitendo cha polisi mara kadhaa kukamata waziri
wa zamani wa smz kumhoji na kushindwa kumfikisha mahakamani kujibu
mashitaka yanayomkabili, Kamanda Msangi alisema kukanatwa au kuhojiwa na
polisi haina maana unakabiliwa na shitaka au kesi mahakamani.
"Tuna uwezo kisheria kumwita mtu tunayemtuhumu kwa sababu kadhaa
kituhuma ili kuchukua maelezo yake,kuhitaji ufafanuzi toka kwake baadae
aidha kumfikisha mahakamani au kumwachia huru hadi wakati muafaka
"alieleza kamanda huyo .
Jeshi la polisi mapema wiki yq jana kilisema limemeita katibu mkuu wa
cuf maalim seif ili kumhoji kwa msuala kadhaa jambo ambalo hadi sasa
mahijiano hayo yamekwama kufanyika.
Macho na masiko ya wengi wanatia shaka huenda kiongozi huyo kuitwa kwake
polisi ni kufuatia matamshi yake aliyosema kwamba Rais wa zanzibar Dk
Ali Mohaned shein ni dikteta na hatakaa madarakani na kufika mwaka 2020
viswani humu.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia