SMZ YATOA MAAGIZO MAZITO KWA MA DC NA MA RC PEMBA


Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar(SMZ ) imewaaagiza wakuu wa mikoa na Wilaya kuwachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kuwasimamisha kazi Watumishi  wa Umma wanapuuzia maelekezobya serikalu na badalabyake kuchukua mawazo ya baadhi ya viongozi wa Kisiasa wakati wa kutekelezw majukumu yao.
SMZ A imesema haiwezekani kwa mtumishi wa Umma akaachwa aendelee kupuuza  na kusaliti maelekezo ,  maagizo au  amri zinazotolewa na serikali katika kuwatumikia wananchi huku wakiangalia macho vitendo vya unyanyasaji na ubaguzi vikishamiri ilani watukishi hao wakikipwa  mshahara na  Serikali inayotokana na jasho la wananchi.
Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd ametoa msimamo huo  jana wakati akizungumza na viongozi wa halmashauri za wikaya za CCM toka  Mikoa miwili ya Kusini na Kaskazini Pemba kikao kilichofanyika katika  kiwanda cha Makonyo na Rri ya Mafuta  huko  Wawi Mkoa wa Kusini Pemba.
Balozi Seif alisema taratibu za kuwafukuza  watumishi  waliosimamishwa  na watakaosimamishwa kazi  kwa mujibu wa kanuni, taratibu na sheria za utumishi Serikalini zitafuata hapo baadaye kwa wale watakaoshindwa kubadilika kutokana na kushabikia siasa na kuacha majukumu yao ya ajira
Alieleza kuwa SMZ haiwezi kuvumilia maovu ya watu na hata mtu mmoja atakayoyafanya dhidi ya Serikali huku kitolea mfano matendo ya kuwatenga baadhi ya wananchi na kunyimwa kupatiwa huduma muhimu za kijamii kama usafiri wa baharini,  magari na kukataliwa kununua au kuuziwa bidhaa
"Kuanzia sasa Dc na Ma RC mkimbaini mtumishi wa serikali anasaliti na kupuuza maagizo ya serikali msimakisheni kazi, taratibu na kanuni zitafuata naadae"alisema Balizi seif
Alisema SMZ litahadharisha na kuwaeleza kuwa inaelewa kuwa hali ya mitafaruku kisiwani Pemba ina kuwa kwa malengo maalum na wanasiasa uchwara.  Hivyo kupitia vyombo vya dola alisema italazimika kuimarisha ulinzi ili kuwapa fursa wananchi waendelee kupata wasaa mpana  wa kuishi kwa amani, utulivu na upendo miongoni mwao.
Balozi Seif alisema cheche za shari na uvunjifu wa amani zinazojiri sasa kisiwanibhuku zina dhamira ya wazi ya kutaka jamii ya kimataifa iione Zanzibar kuna  tatizo na vurugu zilizosababishwa na matokeo ya uchaguzi wa mwezi wa oktoba ambao  uliofutwa kisheria na Tume ya Uchaguzi Zanzibar kwa mujibu wa sheria.
"Mfumo wa vyama vingi  Barani Afrika ikiwemo Zanzibar una safari ndefu kueleweka pengine hali hiibkwa Tanzania imethibitishwa na ripoti ya Jaji Francis Nayalali ambapo   wanqnchi asilimia 80 walipinga  vyama vingi na asilimia 20  kutataka mabadiliko ya mfumo wa kisiasa "alikumbusha.
Alisema kujenga chama cha siasa na kukubakika si janbo la kufumba macho na kufumbua hivyo vyama vichanga huwaza kushika madaraka ya utawala na kusahau kujiimarisha na kukubalika kama ilivyo  CCM .
Akizungumzia wananchi waliopatwa na mitihani ya kufanyiwa hujuma mara na baada ya uchaguzi mkuu Balozi Seif alisema Serikali Kuu inafikiria kuangalia namna itakavyoweza kuwasidia wananchi waliohujumiwa mali zao, vifaa na vyombo  vyao vya usafiri.
Alisema nia njema ya seriiali za ccm kukubali kusikiliza hata maoni ya wachache ilibkuruhusu vyama vingi  inayoonekanq kutumiwa vibaya na viongozi  wasaka madaraka kwa hila ,nguvu na matumizi ya siasa za ukabila na mgawanyiko.
Mapema Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum ya SMZ Haji Omar Kheir  aliwahimiza wakuu wa wilaya na mikoa kisiwani humu kutambua kuwa dhamana ya ulinzi wa amani na usalama wa watu iko mikononi mwao  hivyo wana wajibu wa kusimamia kila hatua .
Waziri Haji alisema usimamizi  wao imara wa sera za serikali, maagizo na tataribu za kiutawala na zile za kiutumishi sasa zinahitaji kusimamiwa kwa weledi, umakini  na vitendo kuliko wakati mwingine wowote.
"SMZ inajua na dunia ya wapenda amani inatambua kuwa kuna wanasiasa wapenda madaraka ambao wameshindwa uchaguzi wanachochea ghasia na kueneza sumu ya maneno ili amani, utukivu na uendo vitoweke pemba ili wao wayafikie matlaba yao"alisema  waziri huyo wa smz
Waziri Haji alisisitiza kuwa haipendezi kuona maamuzi mengine na masuala madogo ambayo yako chini ya dhamana ya viongozi hao yakisubiri kuamuliwa au kuchukuliwa hatua stahili na Rais au  Makamu wa Pili wa Rais wakati masuala mengine yao katika uwezo wao.
"Serikali imekupa dhamana ya kiutawala ili kutenda haki mahali stahili lakini msishindwe kufanya maamuzi magumu ikiwa litajitokrza kundi la watu wajaokusudia kuvuruga amani ya nchi na usalama wa watu. "Alisema waziri huyo.
Makamu wa pili wa Rais na msafara wake yuko kisiwani Pemba iliwatembelea wananchi kwa lengo la kuwafariji na kuwapa pole wale ambao mashamba yao na wao wenyewe kudhuriwa na watu ambao hadi sasa hawajajulikana.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post