AFP:MSAJILI AFUTE VYAMA TISHIO KWA AMANI YA TAIFA


 
 PICHA NA MAKTABA
Na mwandishi wetu , Zanzibar
Wakati Chama Cha Wananchi  (CUF) kikijiandaa  kumshitaki Waziri wa Mambo ya Ndani na IGP kwa madai na tuhuma  ya kuhusika na  uvunjaji  haki na uhalifu dhidi ya binadamu Chama Cha Wakulima  (AFP ) kimemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi  kukitazama  CUF kwa jicho la pili.
Aidha  kimesema ikiwa CUF kitakwenda katika  mahakama ya ICC  kwa ajili ya kufungua  mashitaka dhidi ya madai ya uhalifu na uvunjaji haki, chama hicho kitasimama hadharani kuelezea jinsi kilivyoshiriki  kufanya hadaa na udanganyifu  hadi uchaguzi   wa oktoba 25 kuvurugika  hatimaye kufutwa kisheria na Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC ).
Msimamo huo umetolewa  jana na Mwenyekiti wa AFP Taifa Said Soud Saud katika mahojiano na Libeneke la Kaskazini  yaliofanyika nyumbani kwake huko Mombasa Mkoa wa Mjini Magharibi kisiwani Unguja .
Soud alisema chama cha siasa hakiruhusiwi  kususia na kutoshiriki uchaguzi mkuu huku kikitaka kishike madaraka kwa njia za kidemokrasia. AFP kimesema chama kinapokataa kushiriki uchaguzi aidha kitakuwa kinapania kushika madaraka kwa hila au kufanya mapinduzi ambayo ni kinyume na miiko ya demorasia duniani .
Chama hicho  ( AFP) kimemuomba  Msajili wa Vyama vya Siasa nchini  Jaji Francis Mutungi kukitazama upya chama hicho na ikiwezekana alichukulie hatia za kisheria na ikibidi akifute kwenye orodha ya vyama vya siasa .
Soud alitoa tamko hilo kufuatia kutanda kwa kizungumkuti cha  kauli za   Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad  na ile ya Naibu Katibu Mkuu wake zanzibar Nassor Ahmed Mazrui kwa nyakati tofauti huku viongozi hao wakitaka  wananchi wasilipe kodi ,wafanyabiashara kutokata  leseni pamoja na chama hicho  kutaka kufungua kesi mahakama kuu ya Tanzania na ICC washitakiwa wakiwa  IGP na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Soud alisema madai hayo chama chake kinayaona ni ishara ya  kufilisika, kupoteza, dira , kupauka kufikra kwa viongozi wa kisiasa  chama hicho kinachoonekana  kupoteza matumaini  baada ya kususia uchaguzi na sasa kikiwa nje ya medani za serikali.
"Sikutegemea kumsikia Maalim Seif akiwa kiranja wa kuhamasisha wafanyabiashara wasikate leseni  na kutolipa kodi huku  akihimiza wakulima wa  karafuu wasiuze mazao yao serikalini,nafikiri hapa alipofika amemalizika kisiasa na anaonyeshe  uvumilivu wa kisiasa umemshinda "alisema Soud .
Mwenyekiti huyo wa AFP Taifa  akizungumzia kupuuzia  ripoti ya CUF  kuhusu  uvunjaji wa haki za binadamu na dhamira ya kumshitaki IGP na Waziri wa Mambo ya Ndani, alisema huenda madai hayo yanaielekeza jamii kuona jinsi ya kina cha upambanuzi wa mambo ya kisiada , kiuongozi na kimaono yakipunguabkwa viongozi wa cuf na kukosa mipango mbadala  ya  kisiasa "Hakuna mzanzibari mwerevu, muumini wa haki anayeweka  hofu kwa mungu atakayekubali kusimama na kusema ulipia  uvunjaji wa  haki, mateso au vipigo toka jeshi la polisi katika uchaguzi mkuu wa oktoba 25 au hata ule  wa marudio uliofanyika machi 2o mwaka jana " alieleza Soud. Alisema ikiwa CUF kweli  watakwenda ICC  itakuwa ni nafasi ya chama AFP  kupanda kizimbani ili  kutoa ushahidi kamilifu na kuieleza dunia jinsi chama hicho kilivyoshiriki  kutenda hila na udanganyifu katika uchaguzi mkuu hususan  Pemba hadi ZEC ikafuta matokeo ambayo yalikiuka taratibu za kidekokrasia.
"Hatuungi mkono na wala hatutaunga mkono   siasa  za kitoto  kwasababu madai yao yamekosa msingi na hayana mantiki " alisisitiza .
Mwenyekiti huyo wa AFP alisema  ni ajabu kuona  CCM  na CUF  walipounda serikali ya Umoja wa Kitaifa bila kuvishirikishs vyama vingine kwa miaka mitano , Maaalim Seif na washirika wake walikataa kimya na hawakukutokea sekeseke wala sokomoko  ,lakini baada ya kuona AFP , ADC na TADEA vikishirikishwa serikalini ,vigogo wa CUF   udenda unawatoka huku milango ya kuingia serikalini ikiwa   imefungwa na haifunguki tena.
Aidha Soud alikana kuwa Maalim  Seif kama kwelibalishinda uchaguzi  wa oktoba 25  mwaka jana  kwa kuwa mshindi halali wa uchaguzi aliwwma si mtu  kujitangaza   mwenyewe bila kutangazwa na chombo chenye dhamana ya kikatiba  kisheria.
"Tunamtahadharisha Msajili wa vyama vya siasa  kwamba chokochoko za viongozi wa CUF huenda zukazuia jambo  usoni kwani aina ya siasa hizo ziliyaingiza mataifa ya Kenya, Burundi na Rwanda katika vita ya kikabila na kuzuka mapigano ya wenyewe kwa wenyewe  yaliosibajisha mauaji ya kimbari na mamilioni ya watu kupotea " alieleza . Alisema Si CUF tu hata AFP kama kitashiriki siasa za ubaguzi,kuigawa jamii na kuwahasimisha watu  wasizikane,  kifutwe kwa mujibu wa sheria kwani kiongizi au chama kushiriki uchochezi wa aina hiyo ni kwenda kinyume na sheria No 5 ya mwaka 1992.
"Huwezi kukiacha chama kikieneza  na kuhubiri misingi ya ubaguzi, imani za dini , uzawa , nasaba na asili za  watu bila ya kukidhibitiwa au kutokichukulia hatua mahususi za kisheria  .
"Maalim Seif ifike mahali akomae kisiasq kama mwenzake  Edward Lowassa wa Chadema, ameshindwa uchaguzi mkuu amekubali matokeo sasa anajipanga upya kushiriki siasa  mwaka 2020, kulalamika kwake kuhusu uchaguzi wa Zanzibar mwaka 2015  hakutamsaidia lolote . "Alisema Akizungumzia uamuzi wa Rais kumteua na kufanya kazi katika SMZ akiwa Waziri Asiye na Wizara Maalum  , Soud alimsifu Rais Dk  Shein kwa kujua kwake jinsi ya kutenga wakati wa kisiasa na ule wa utendaji kiserikali hukubakisisitiza kuwabunapowakuta mawaziri kwenye Baraza la Mapinduzi huwezi kueleza kama kuna mawaziri toka upinzani na chama tawala.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post