AWUSA YAANZISHA ULIPIAJI WA ANKARA KUPITIA MITANDAO YA SIMU

Mamlaka ya maji safi na maji taka jijini Arusha [AWUSA] wameanzisha
huduma ya kulipa bili ya malipo ya Ankara kwa wateja kupitia mitandao
yote ya simu za mikononi.

Akizungumza na Nipashe mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja  Masoud
Katiba katika maonyesho ya wakulima na wafugaji TASO nane nane,alisema
kuwa mamlaka ya maji safi na maji taka jijini Arusha limeamua kuweka
huduma hiyo ili kuweza kulipa bili zake kwa wakati unaotakiwa.

Aidha alisema kuwa sababu nyingine ya kuweka huduma hiyo ni ili
kumrahisishia mteja wake katika kupunguza muda mwingi wakati wakulipa
Ankara zake,na kutembea muda mrefu kuzifuata huduma hizo na kuepukana
na usumbufu unaoweza kujitokeza.

Masoud aliongeza kuwa mitandao itakayotumika katika kurahisisha huduma
za mamlaka ni pamoja na M-PESA,TIGO PESA,AIRTEL MONEY ambapo amesema
mpaka sasa asilimia 10 ya wateja wameanza kulipia bili zao kwa kutumia
mtandao wa M-PESA ambapo amesema ndani ya mitandao yote kuna namba
maalumu ambazo mteja anaweza kuzitumia

Aidha alibainisha kuwa njia  hii itamsaidia mwanananchi kuokoa muda na
fedha nyingi ambazo alikuwa akiutumia kwa ajili ya kwenda idara ya
maji badala  yake anatumia kwa kufanyia kazi nyingine.
“tumeanzisha hii ili kumraisishia mteja kulipa bili yake kwa wakati
nabila usumbufu wowote napia na sisi kama idara ya maji tunatakiwa
tuende na wakati hasa katika kipindi hichi cha digital”alisema Masoud

Alitoa wito kwa wananchi kuepuka na usumbufu wa kwenda kulipa bili zao
za maji (Ankara)katika ofisi na badala yake watumie huduma hizi mpya.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post