SEREKALI YAPOTEZA KODI NYINGI

Mbunge  wa EALA, Shy-Rose  Bhanji akichangia mada ndani ya bunge hilo

Na Woinde Shizza,Arusha



 Serekali imekuwa inapoteza kodi nyingi  zinazotokana  na ushuru wa mazoao kutokana na kuwa na mzabuni  mmoja ambaye anakusanya  kodi za mazao  kwa nchi nzima .

Hayo yamebainishwa na  mbunge wa  EALA, Shy-Rose  Bhanji wakati akiongea na waandishi wa habari ndani ya viwanja vya bunge hilo   ambapo alisema kuwa kuna changamoto kubwa  ya utekelezaji wa umoja wa forodha hapa nchini Tanzania.

Alisema kuwa  wafanyabiashara wengi pamoja na wakulima ambao wanazalisha mazao pamoja na bidhaa mbalimbali  zinazofikia kiwango   staili cha asilimia 50 %hadi 100% wanakuwa awatozwi kodi wakati wanapeleka bidhaa zao katika  nchi za jumuiya wanachama .

 Aidha alibainisha kuwa kuna tatizo kubwa kwa upande  wa Tanzania kwani hati ambazo zinatolewa kwa ajili ya kukusanya kodi  au kubaini viwango vya kusamehewa kodi zinatolewa na taaasisi moja tu ambayo ni ya tccia.

Alisema kuwa hili ni tatizo ambalo linatakiwa kutazamwa  upya katika nchi yetu na serekali kwasababu TCCIA aipatikani nchi nzima bali inapatikana katika baadhi ya sehemu ambayo ni mikoa tu  huku katika ngazi za wilaya pamoja na vijiji awapatikani.



Alisema kuwa hii inapelekea kodi nyingi ya mazao kupotea na pia wananchi wengi  pamoja na wafanya biashara wengi kutokujua dhamana ya kodi ambayo inaweza kumuwezesha mfanyabiashara kujua unafuu wa wa kodi.



“sasa ivi ili kuweza kuwapa nafasi wananchi wengi pamoja na wafanyabishara wengi ili waweze kuelewa  dhana ya unafuu wa kodi ,ni jukumu la serekali kutoa jukumu la kutoa hati  hizi kwa wadau wengine ili kuleta unafuu wakodi “alisema Bhanji



Aidha alisema kuwa ili kurahisisha mambo ni vizuri ofisi za biashara za manispaa pamoja na  ofisi za biashara za  wialaya nawao waweze kupewa  ili jukumu na wao waweze kutoa hati ambazo zitawapa nafasi wafanya biashara ambao wanasifa zinazokithi maitaji na wenye sifa kuweza kupata hati hizo .

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post