Ticker

6/recent/ticker-posts

WALIOKUWA MADIWANI WA CHADEMA WALIPISHWA FAINI YA MILIONI 15 NA MAHAKAMA WAKISHINDWA KULIPA KWENDA MAGEREZA



HATIMAYE hukumu ya  kesi ya madai iliyokuwa ikiwakabili  waliokuwa
madiwani watano wa  chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) hukumu
yake imesomwa ambapo mahakama imeamuru madiwani hao kulipa kiasi cha
shilingi milioni 15 kwa awamu mbili na endapo kama watashindwa kulipa
fedha hizo basi watapelekwa magereza

Akitoa hukumu hiyo mbele ya Umati wa watu ambao walikuwa wamefurika
mahakamaani hapo mapema jana katika mahakama kuu kanda ya Arusha
Charlz Magesa alisema kuwa rufaa imefika mwisho

Magesa alisema kuwa washitakiwa hao ambao  walikuwa madiwani wa kata
tano za jiji la Arusha wamekutwa na hatia hivyo mahakama imeamuru
walipe kiasi hicho cha fedha haraka iwezekanavyo na endapo kama
watashindwa kufanya hivyo basi watachukuliwa hatua kali ikiwemo
kupelekwa magereza.

Aliongeza kuwa kwa sasa Madiwani hao wanatakiwa kulipa fedha hizo kwa
awamu mbili ambapo awamu ya kwanza itakuwa ndani ya wiki mbili wakati
awamu ya pili itakuwa ya mwisho na nibaada ya miezi miwili.

‘kwa sasa mnatakiwa muhakikishe kuwa mnalipa fidia kwa haraka sana na
kama mtashindwa kufanya hivyo basi mahakama itachukua hatua na
maambuzi makali zaidi ya haya’aliongeza Magesa

Wakiongea nje ya mahakama mara baada ya kukubaliana kulipa kiasi hicho
cha fedha madiwani hao ambao walikuwa mahakamani hapo ambao ni Rehema
Mohamed,Charlz Mpanda,na Rubeni Ngowi walidai kuwa Chadema
haiyawatendea haki kwa kuwa fedha ambazo wanatumia kumlipa Wakili ili
kuwakandamiza ndizo walizozitafuta kwa kipindi cha hapo awali.

Madiwani hao waliongeza kuwa wao wapo tayari kulipa hizo gharama kwa
ndiyo haki ambayo Chadema walikuwa wanaililia hivyo wameomba Viongozi
wa Taifa watafute njia nyingine ya kutatua migogoro na wala sio
kufukuza  kwani inapoteza imani na chama

‘ukiangalia hapa tunaambiwa kuwa tulipe kiasi hiki cha fedha lakini
nguvu zetu bado hazijalipwa na sisi ndio tuliotangaza Chadema kwa mkoa
wa Arusha na mpaka sasa Kila mtu anaijua Chadema lakini malipo yake
ndiyo haya sisi tunasema kuwa huu si mwisho wa siasa bado tupo na
tutakutana katika gemu nyingine ‘waliongeza madiwani hao

Pia walisema kuwa pamoja na kuwa baadhi ya waliokuwa madiwani hawataki
siasa lakini bado wengine wataendelea tena kwa kishindo kikubwa hata
kama Chadema wanadai kulipwa fedha zao na kata zao zikiwa zinabaki
hazina madiwani kwa muda mrefu sana.

Awali Kesi hiyo ilitokana na madiwani hao kufungua kesi ya kupinga
kufukuzwa na kuvuliwa uanachama baada ya kudaiwa kukiuka sheria na
kanuni za chama, zikiwemo sheria za kuwataka kutoingia katika vikao
vya madiwani vya Jiji la Arusha kwa madai ya kutomtambua Meya wa
Arusha Gaudence Lyimo wa Chama cha Mapinduzi(CCM)

Post a Comment

0 Comments