Mwenyekiti wa bodi ya benki ya KCB Tanzania,Bw.Edmund
Mndolwa katikati akimkabidhi moja ya msaada wa madawati kati ya 89 Mwalimu Mkuu
wa shule ya Msingi ya Makumbusho Bi.Benedicta Lyimo,yaliyotolewa na benki hiyo
yenye thamani ya Milioni 17.4,anaeshuhudia kulia ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano
wa benki hiyo Bi.Christine Manyenye.
) Mwenyekiti wa bodi ya benki ya KCB Tanzania,Bw.Edmund
Mndolwa kushoto na Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo Bi.Christine
Manyenye wakioneshwa moja ya jengo la wodi ya kujifungulia wakinamama na Mganga
Mkuu wa Hospitali ya Sinza Dare s Salaam mara baada ya kukabidhi rasmi vifaa
mbalimbali vikiwepo vitanda vya kujifungulia vine vyote vikiwa na thamani ya
Milioni 7.4 kwa ajili ya kituo hicho.
Mwenyekiti wa bodi ya benki ya KCB Tanzania,Bw.Edmund
Mndolwa akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki
hiyo Bi.Christine Manyenye,wakati alipokuwa akikagua moja ya vitanda
kati ya vinne vya kujifungulia wakina mama kabla ya kuvikabidhi rasmi
kwa uongozi wa Hospitali ya Sinza iliyopo jijini Dar es Salaam vyote
vyenye thamani ya shilingi milioni 7.4 ,kushoto Meneja Masoko wa benki
hiyo Emelda Gerald.
Mwenyekiti wa bodi ya benki ya KCB Tanzania,Bw.Edmund
Mndolwa akisalimiana na mmoja wa
wanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Makumbusho alipofika shuleni hapo
kutoa msaada wa madawati 89 na vifaa vya kusomea,vyote vyenye thamani
ya shilingi milioni 17.4 kulia ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo
Bi.Christine Manyenye.
Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki ya KCB Tanzania
Bi.Christine Manyenye na Meneja Masoko wa benki hiyo Emelda….wakimsikiliza
Muuguzi wa Hospitali ya Sinza jijini Dar es Salaam Rachel Mshana mara
walipofika hospitalini hapo kukabidhi msaada wa vitanda vine na vifaa mbalimbali
kwa ajili ya kujifungulia akinamama wajawazito vyote vyenye thamani ya shilingi
milioni 7.4.
Mwenyekiti
wa bodi ya benki ya KCB Tanzania,Bw.Edmund
Mndolwa kulia akimkabidhi moja ya msaada wa madawati na meza Mwalimu
Mkuu wa shule ya Msingi Kibamba yenye watoto wenye ulemavu wa akili
Bi.Asia
Mpate,yaliyotolewa na benki hiyo yenye thamani ya Milioni 17.4,katikati
ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo
Bi.Christine Manyenye.
Mwenyekiti wa bodi ya benki ya KCB Tanzania,Bw.Edmund
Mndolwa akimkabidhi Mganga Mkuu wa
Hospitali ya Sinza ya jijini Dares Salaam,Benedict Luoga moja ya kitanda kati
ya vinne Salaam vyote vyenye thamani ya shilingi milioni 7.4 vilivyotolewa na
benki hiyo kwa ajili ya kujifungulia akinamama wajawazito.
Mwenyekiti wa bodi ya benki ya KCB Tanzania,Bw.Edmund
Mndolwa kulia akimsikiliza jambo Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kibamba yenye watoto wenye ulemavu wa akili Bi.Asia
Mpate,baada ya kumkabidhi rasmi msaada wa madawati 89 yenye thamani ya Milioni
17.4,wapili kulia k Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo Bi.Christine
Manyenye,na kushoto ni Mwalimu msaidizi wa shule hiyo Bi.Mwajabu Minja.
Na Mwandishi wetu
Shule
ya Msingi ya Kibamba katika wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam
inakabiliwa na uhaaba wa madawati 500, jambo linalowalazimu wanafunzi
wa shule hiyo kukaa chini wakati wakifundishwa darasani.
Mwalimu
Mkuu wa shule hiyo, Asia Mpate alibahanisha hayo jana na kusema kuwa
shule yake yenye wanafunzi 1,950,kuliwa na madawat 320 na madarasa 13
tu.
Mwalimu
Mkuu huyo alikuwa akizungumza kwenye hafla ya kukabidhiwa misaada na
Benki ya KCB iliyotoa madawati 25, meza tatu, viti vya walimu sita,
madafyari 235 na peni 200 , vyote vikiwa na thamani ya Sh, Milioni 5 kwa
shule hiyo.
Alisema
kuwa uhaba mkubwa wa madawati katika shule yake kumepelekea utoro
mkubwa kwa wanafunzi wake kwani wanafunzi wake hulalamikia hali mbaya
na ugumu wa kukaa chini sakafuni.
Mpate
amesema kuwa wanafunzi wengi wa shule yake wamechanganyikiwa na hali
hiyo na hivyo huamua kutohudhuria masomo, jambo linaofanya ufanisi
mdogo wa elimu kwa wanafunzi wake.
"
Utoro ni mkubwa katika shule yetu kwa sababu hali halisi ya madarasa ni
ya kutisha, hatuna madarasa ya kutosha wala vitendea kazi .
Tunashukuru Benki ya KCB kwa msaada wao ambao tunaamnini kuwa
utatusaidia kuboresha kiwango cha elimu katika shule yetu", alisema
mwalimu mkuu huyo..
Kwa
upende wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo, Dk
Edmund Mndolwa alisema kuwa msaada huo ni sehemu ya wajibu wake wa
benki kusaidia jamii na kwamba benki yake imejidhatiti kusaidia kuinua
kiwango cha elimu nchini Tanzania.
Aliwashauri wanapokea misaada ya benki hiyo kutumia ipasavyo na inavyotakiwa misaada inayotolewa na benki yake.
Kwenye
hafla hiyo pia benki ya KCB ilitoa msaada wa madawati 64 yenye thamani
ya Sh. Milioni tano kwa Shule ya Msingi ya Makumbusho pia ya jijini.
Wakati
huo huo hopsitali ya Sinza ya jijini Dar es Salaam imepokea msaada
wa vifaa vya hospitali vyenye thamani ys Sh. Milioni 7.4 kutoka kwa
Benki ya KCB katika hafla iliyofanyika kwenye hopsitali hiyo jana.
Dokta
Mwandamizi wa hospitali hiyo, Dk Benedict Luwoga alishukuru benki
hiyo kwa msaada huo na kusema kuwa vifaa hivyo vilikuja kwa wakati na
kuvitaja vifaa hivyo ni pamoja na vitanda vinne vya kuzalisha kwa
mama wajawazito.
Alisema
kuwa hospitali yake ilizidiwa uwezo kwa sababu ilikuwa na vitanda
viwili tu vya kuzalisha mama wajawazito , kwa hiyo vitanda hivyo vinne
zaidi ilikuwa ni ukombozi mkubwa kwa hospitali yake.
"Tunashukurui
Benki ya KCB kwa msaada huo, umekuja kwa wakati ambapo hospitali
ilikuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi. Amezitaka kampuni zingine
ziige mfano wa benki ya KCB", alisema Dk Luwoga.