PIcha juu na chini ni Miongoni mwa nyara za serekali zilizokuwa
zimehifadhiwa kwenye ghala maalumu kwenye nyumba ya mtuhumiwa Peter
Lawrence zikionekana kwenye maboksi tayari kwa kusafirishwa nje ya
nchi.
zimehifadhiwa kwenye ghala maalumu kwenye nyumba ya mtuhumiwa Peter
Lawrence zikionekana kwenye maboksi tayari kwa kusafirishwa nje ya
nchi.
ngozi ya mamba ambayo ilikutwa kwenye ghala la mtuhumiwa
ikiwa ni sehemu ya nyara mbali mbali zilizokutwa kwenye ghala hilo
ikiwemo meno ya tembo,vichwa vya simba,vichwa vya nyati,ngozi ya
simba,ngozi ya tembo na nyara nyingine nyingi za wanyama mbali
mbali.(picha zote na mahmoud ahmad arusha)
ikiwa ni sehemu ya nyara mbali mbali zilizokutwa kwenye ghala hilo
ikiwemo meno ya tembo,vichwa vya simba,vichwa vya nyati,ngozi ya
simba,ngozi ya tembo na nyara nyingine nyingi za wanyama mbali
mbali.(picha zote na mahmoud ahmad arusha)
Mtuhumiwa wa nyara za serekali Peter Laurence mwenye kofia
katikati akiwa na maofisa wa jeshi la polisi chini ya ulinzi ,eneo la
kisongo mtaa wa mateves nje kidogo ya jiji la Arusha baada ya
kukamatwa na shehena ya nyara za serikali nyumbani kwake
katikati akiwa na maofisa wa jeshi la polisi chini ya ulinzi ,eneo la
kisongo mtaa wa mateves nje kidogo ya jiji la Arusha baada ya
kukamatwa na shehena ya nyara za serikali nyumbani kwake
JESHI la polisi mkoani Arusha,limekamata shehena
kubwa ya nyara mbalimbali za serikali zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye ghala
maalumu,eneo la Matevesi Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha,zikiwa tayari kwa
kusafirishwa nje ya nchi.
Nyara hizo ni pamoja na Ngozi za Simba,Chui na Mamba
,meno ya Tembo,vichwa vya Nyani,Swala na Nyati,Pembe za kifaru,na zingine
nyingi ambazo jeshi la polisi linaendelea kuzitambua.
Sambamba na hilo jeshi hilo limemtia mbaroni
mtuhumiwa wa nyara hizo aliyetambulika kwa jina la Peter Leurence (55)mkazi
Ngaramtoni ya chini,ambaye alikuwa akiwa amezihifadhi kwenye maboksi zaidi ya
20,kwenye nyumba yake iliyopo eneo hilo.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoni
Arusha,Liberatus Sabas tukio la kukamatwa kwa nyara hizo limetokea jana majira
ya saa 6.30 usiku wa kuamkia leo eneo la
kisongo mtaa wa mateves baada yak upata taarifa kutoka kwa raia wema.
Kamanda Sabas alisema kuwa baada ya jeshi hilo kupata
taarifa za siri majira ya saa 5 asubuhi walifika eneo la tukio majira ya saa 7
mchana na kupata upinzani mkubwa kutoka kwa walinzi wa wanaolinda eneo hilo kwani
waliwanyima kuwapa maelekezo ya kumpata mmiliki wa nyumba hiyo.
Hata hivyo alisema kwamba askari hao waliamua
kumueka chini ya ulinzi kwa kumshurutisha mlinzi mmoja iliaweze kuwapa ushirikiano
ambapo aliwapaita namba za simu na mtuhumiwa aliwaambia kuwa yupo magugu mkoani
Manyara na angefika saa 12 majira ya jioni.
Taarifa zinadai kuwa baada ya mtuhumiwa kufika
jitihada za kufanya upekuzi zilifanyika chini ya polisi wenye silaha za moto na
walikuta shehena kubwa ya nyara za serekali zilizokuwa zimahifadhiwa kwenye
ghala maalum na kufungwa kwenye mabox teyari kusafirishwa kwenda kusikojulikana.
Alisema kuwa polisi waliamua kuweka ulinzi hadi
kulipokucha na huku wakiendelea kumshikilia mtuhumiwa huyo na jeshi hilo linaendelea kumshikilia
mtuhumiwa huyo pamoja na watoto wake wawili waliokutwa wakiishi kwenye nyumba
hiyo.
Aidha kamanda Sabas alisema kuwa kesho yake polisi
waliendelea kufanya upekuzi na kubaini mabox zaidi ya 20 yenye nyara mbali
mbali miongoni mwa nyara hizo alizitaja kuwa ni Ngozi za Chui.Simba,Tembo na
Mamba pia kulikuwemo vichwa vya nyani,chui,swala nyati,pembe za faru ,meno ya
tembo na nyingine nyingi ikiwemo mfuko wa silaha inayosadikiwa kuhifadhia
silaha.
Kwa mujibu wa
kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa alisema kuwa Watuhumiwa bado
wanashikiliwa na jeshi hilo kwa mahojiano na watafikishwa kwenye mahakama pindi
upelelezi wa tukio hilo utakapo kamilika.