TAHADHARI YA MVUA KUBWA KUNYESHA



Tafadhali pokea taarifa hii kuhusu uwezekano wa matukio ya Mvua kubwa
(zaidi ya milimita 50 katika kipindi cha saa 24 kila siku) katika baadhi
ya maeneo ya mikoa  ya Rukwa, Iringa, Mbeya, Njombe, Ruvuma, Morogoro,
Pwani, Lindi, Mtwara  na maeneo jirani ya mikoa hiyo kati ya tarehe 30
Januari, 2013 hadi 01 Februari, 2013.

Hali hii inatokana na kuwepo kwa kimbunga “FELLENG” kaskazini-mashariki mwa

Madagascar ambacho kinavuta upepo wenye unyevunyevu kutoka Congo kupitia
maeneo tajwa.
 Pokea taarifa hii ya tahadhara ya uwezekano wa kuwepo kwa mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo nchini kutokana na kimbunga FELLENG.
Mamlaka inaendelea kufuatilia hali hiyo
Naambatanisha taarifa kamili pamoja na satelite picha ya hali inavyoonekana wakati taarifa hii ikitolewa
Monica Mutoni
Kaimu Meneja Mahusiano
TMA

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post