Meneja wa bia ya Guinnes Davis Kambi akipiga picha ya pamoja na washiriki wa shindano la Guinness Football Challenge wakati walipokuwa wakiagwa kwenye mgahawa wa City Sports Lounge Posta jana jijini Dar es salaam, washiriki hao wameondoka usiku wa kuamkia leo kuelekea nchini Afrika Kusini ambako watashiriki katika shindano hilo.
Meneja wa bia ya Guinnes Davis Kambi akiwaaga rasmi washiriki wa shindano la Guinness Football Challenge wakati akiwaaga kwenye mgahawa wa City Sports Lounge usiku wa kuamkia leo jijini Dar es salaam.
Mwanablogu Wiliam Mlecela Le Mutus akishoo love na washiriki wa shindano la Guinness Footbal Challenge jana usiku wakati walipoagwa rasmi.
Mablogger wakishoo Love mbele ya Camera ya Fullshangweblog kutoka kulia ni Othman Michuzi, Henry Mdimu, John Bukuku, Ahmde Michuzi, William Malecela Le Mutus, Josephat Lukaza. Francis Dande, Kassim Mbarouk na Mroki Mroki aliyekaa chini.
Wadau Wakili Michael Ngaro na Sebo wakijadiliana jambo wakati wa hafla hiyo kwenye mgahawa wa City Sports Lounge jana usiku.
Mkurugenzi wa Kampuni ya R&R Bi. Caroline Gull akijadiliana jambo na Peter Ngasa Meneja wa Kampuni ya R&R, katikati ni Davis Kambi Meneja wa bia ya Guinness.
Mkurugenzi wa Kampuni ya R&R Bi. Caroline Gull kulia na Regina Gwae Ofisa kutoka Kampuni hiyo wakihakiki moja ya Tiketi za ndege kwa ajili ya washiriki wa Guinnes Football Challenge wakati walipokuwa wakiagwa rasmi jana.