Hollande ahofia ulipizaji kisasi

Rais Francois Hollande wa Ufaransa anasema kuwa atazidisha ulinzi nchini Ufaransa kuepusha mashambulio yanayoweza kufanywa na wapiganaji wa Kiislamu kulipiza kisasi kwa Ufaransa kuingilia kati kijeshi nchini Mali na Somalia.
Rais Hollande akitoa taarifa kuhusu Mali katika ikulu
Bwana Hollande alisema majengo ya serikali na miundo mbinu ya usafiri italindwa zaidi .
Nchini Mali wanajeshi wa Ufaransa wanaendelea kuwashambulia wapiganaji kwa ndege.
Bwana Hollande alisema Ufaransa imesababisha hasara kubwa kwa maadui nchini Mali, lakini kazi haikumalizika.
Jumuia ya nchi za Afrika magharibi, ECOWAS, itatuma wanajeshi huko piya katika siku kumi zijazo.
Mwakilishi wa ECOWAS mjini Bamako, Abdoudou Touré Chéaka, alisema ECOWAS itatuma wanajeshi 2000 kwanza na mwishowe watakuwa 3300.
Alisema wanatarajiwa kuwako huko kwa mwaka mmoja:
"Unapoanza vita unajua vinapoanza lakini hujui lini vitamalizika.
Lakini azimio la Umoja wa Mataifa nambari 2071 limetoa idhini ya mwaka mmoja.
Yaani ikiwa tutafanikiwa kufikia lengo ambalo linajulikana.
Lazima tufanye kila tuwezalo kuikomboa Mali kutoka kwa magaidi, makundi ya wahalifu, na ardhi ya Mali iwe moja tena.
Kama tutafikia lengo katika mwaka mmoja basi tutafuata ratiba, ama sivyo tutakishirikiana na Mali kutafuta suluhu."
Na Uingereza imesema kuwa itasaidia kusafirisha wanajeshi hadi Mali lakini haitashiriki kijeshi.

CHANZO BBC SWAHILI

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post