Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mh.Nyirembe Munassa akifungua mkutano leo(Picha na jamii blog)
Imeelezwa kuwa kukuwa kwa uchumi
duniani hasa kwa nchi zinazo endelea kunategemea njia bora za utunzaji
wa mazingira kwa kuzingatia uzalishaji bora wa viwanda unaoendana na
viwango vya kimataifa
Hayo yameelezwa jijini Arusha
leo wakati wa mkutano wa viongozi wa kimataifa wanaoshughulikia viwango
vya maswala ya mazingira duniani,ambapo mgeni rasmi katika mkutano huo
alikuwa mkuu wa wilaya ya Arumeru Mh.Nyirembe Munassa
Nyirembe Munassa amesema nchi za
dunia ya tatu ziko katika hali mbaya zaidi kutokana na uwezo duni wa
kupambana na athari za mabadiriko ya tabia nchi
Nae mwenyekiti wa mkutano huo
Prof. Robert Page amesisitiza kuanzishwa kwa mkakati madhubuti wa
kupunguza athari hizo kutokana na kwamba maendeleo ya kiuchumi yoyote
hutegemea kwa kiasi kikubwa mazingira yaliyo tunzwa vizuri
Mkutano huo ni wa siku mbili
unaoshirikisha wataalamu wa viwango na wadau wa mazingira duniani,
pamoja na mambo mengine utajadili mpango wa kuwa na teknolojia safi
katika uzalishaji wa bidhaa mbalimbali duniani kote
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi ktika hotel ya Naura spring jijini Arusha
Baadhi ya washiriki wakiwa wanafatilia mkutano kwa ukaribu