Habari zilizotufikia hivi punde zinadai kuwa mwigigizaji nyota katika
tasnia ya filamu Swahiliwood Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameachiwa kwa
dhamana na Mahakama kuu ya Tanzania, taarifa za awali zimedai kuwa
msanii huyo ameachiwa kwa dhamana ya shilingi 20, Lulu alikuwa
akishikiliwa mahabusu katika gereza la Segerea jijini Dar es Salaam.
Wiki iliyopita mawakili wa muigizaji huyo waliwasilisha maombi ya dhamana kwa mahakama hiyo kuu ya Tanzania
Wanasheria hao Peter Kibatala, Kennedy Fungamtama na Fulgence Massawe waliomba dhamana hiyo itolewe haraka kwa kuwa muombaji amekaa mahabusu kwa zaidi ya miezi saba na kwamba kosa lake linaweza kupewa dhamana.
.
Lulu anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia marehemu Steven
Kanumba April 7, 2012, huko Sinza Vatican, jijini Dar es Salaam, Kanumba
alidaiwa kuwa kwenye ugomvi na Lulu aliyekuwa mpenzi wake nyumbani kwa
marehemu Kanumba Sinza Vatcan.