WACHEZAJI WA YANGA WAANZA MAZOEZI BAADA YA KUTOKA UTURUKI


 
Wachezaji wa Young Africans walipokuwa mazoezin katika mji wa Antalya nchini Uturuki
Timu ya Young Africans imeanza mazoezi leo asubuhi katika uwanja wa Kijitonyama mabatini kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu ya vodacom na mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Black Leopard kutoka nchini Afrika Kusini siku ya jumamosi mchezo utakaofanyika katika Uwanja wa Taifa jijiji Dar es salaam.
Young Africans ambayo imerejea siku ya jumatatu alfajiri ikitokea nchini Uturuki ambako ilikuwa imeweka kambi ya mafunzo kwa takribani wiki mbili, iliwapa wachezaji wake mapumziko ya siku mbili kabla ya leo tena wachezaji wote  kuanza mazoezi.
Wachezaji wote waliokuwa na timu katika kambi ya mafunzo nchini Uturuki wameanza mazoezi huku umati wa watu wengi ukijitokeza kuwaona vijana wa Jangwani ambao tangu warejee nchini leo ndio ilikua wanaanza mazoezi katika ardhi ya nyumbani.
Mchezo wa jumamosi dhidi ya timu ya Black Leopard utakua ni mchezo wa kwanza kwa Young Africans katika aridhi ya nyumbani katika mwaka mpya wa 2013 hivyo watatumia fursa hiyo kuwaonyesha washabiki ufundi walioupata kutokana na kambi hiyo ya mafunzo mjini Uturuki.
Timu ya Black Leopard inatajiwa kuwasili siku ya alhamis asubuhi ikitokea nchini Afrika Kusini tayari kabisa kupambana na mabingwa mara 23 wa ligi kuu ya Tanzania bara na mabingwa mara tano (5) wa kombe la Kagame.
Yanga itaendelea na mazoezi yake kesho asubuhi katika uwanja wa Mabatin Kijitonyama kujiandaa na mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa mzuri wenye upinzani na wakuvutia ikizingatiwa timu ya Yanga ilikuwa kambi ya mafunzo nchini Uturuki ambao ilipata nafasi ya kuwa pamoja na mwalimu kuwafundisha wachezaji wake pamoja.
Viiingilio vya mchezo huo ni Tsh 30,000/= VIP A, Ths 20,000/= VIP B, Tsh 15,000/= VIP C , Tsh 7,000/= Orange na Tsh 5,000/= Blue & Green.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post