No title


Na Haruni Sanchawa

SAKATA la mdogo wa Mbunge wa Kinondoni, Seleman Ally Mohamed kudaiwa kumtupia vyombo nje mkewe, Asma Ally limepata ufumbuzi baada ya mmiliki halali wa nyumba waliyokuwa wakiishi wanandoa hao kutinga katika ofisi za gazeti hili na kuanika ukweli.
Seleman Ally Mohamed akiwa na mkewe, Asma Ally.
Mmiliki huyo aitwaye Uddy Juma Boma alitinga katika ofisi zetu Bamaga, Mwenge jijini Dar Alhamisi iliyopita na kuonesha vielelezo vya umiliki wa nyumba hiyo Block D plot Na.382 iliyoko Sinza jijini Dar.
 Katika maelezo yake Uddy alisema kuwa aliinunua nyumba hiyo kutoka kwa mzee Patrick Lence Kimolo mwaka 1995 kwa shilingi  milioni 7 kwa kulipa  fedha katika mahakama ya Magomeni jijini Dar kwa awamu mbili.
“Mwaka 1996 nilihamia na kupokelewa na  mjumbe Ally  Kuza aliyekuwa mwenyeji wangu,“ alisema.
Uddy alisema mwaka 2000 alihamia Bahari Beach katika nyumba nyingine na hiyo ya Sinza akaipangisha kwa Seleman ambaye ni mdogo wa mbunge wa Kinondoni
(Mheshiwa Idd Azzan) kwa shilingi 150,000 makubaliano yalifanyika kwa wakili Godfrey Boniphace Taisamo.“
Mwaka 2006 Seleman alisema kuwa hana uwezo wa kupanga kutokana na gharama za maisha kupanda, cha kushangaza mkewe Nasma amekataa kutoka ndani ya nyumba akidai kuwa ni ya mumewe.
“Mwaka 2009 kesi ilifika mahakama ya nyumba Magomeni mwaka 2011 ikahamia Kinondoni na wakati wote huo Selemani alikuwa akikiri mahakamani kwamba mkewe hataki kuhama,  mahakama ikatoa samansi ya kumuita Asma,“  alisema.
Januari 14, 2013 mahakama ikitoa kibali cha kumtolea  vyombo nje.

ASMA ALLY ANASEMAJE
Asma amemwambia mwandishi wetu kuwa haamini kama nyumba  hiyo siyo ya Selemani kwa sababu walinunua mwaka 2002.
“Mume wangu ametumia mbinu ili kunitimua katika nyumba baada ya kufanikisha kuwachukua watoto na kwenda kuwaficha kwa ndugu zake.
“Wamenifanyia hila ili niweze  kuishi kwa shida, nitaendelea kufuatailia suala hili hadi kieleweke,“ alisema Nasma.

MSIKIE SELEMANI
“Mimi nilikuwa mpangaji tu  na alichokifanya mzee Uddy Juma ni kufuata taratibu ili kuchukua nyumba yake, ni kweli baada ya huyu mwanamke hataki kutoka, niliamua kuwachukua watoto wangu ili yeye ajue namna ya kufanya,“ alisema Seleman.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post