Mkuu wa
chuo cha VETA kipawa, Jijini Dar es Salaam, Eng. Lucius Luteganya,
akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ulipaji ada kwa
wanafunzi wa chuo hicho kupitia huduma ya M – Pesa. Kufuatia
ushirikiano kati ya chuo hicho na Vodacom Tanzania. Kushoto ni Mkuu wa
ukuzaji biashara – M - PESA Jackson Kiswaga.
Meneja
mawasiliano wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa, akimuelezea jambo Mkuu wa
Chuo cha Veta Kipawa, Eng. Lucius Lutenganya wakati wa uzinduzi wa
ulipaji ada kupitia huduma ya M – pesa kwa wanafunzi wa chuo hicho.
Katikati ni Mkuu wa Ukuzaji Biashara – M - PESA, Jackson Kiswaga.
Wanachuo
wa Chuo cha VETA Kipawa Dar es Salaam kuanzia sasa wataanza kulipa ada
kupitia huduma ya M-Pesa baada ya chuo hicho kufikia makubaliano na
Kampuni ya Simu za mikononi ya Vodacom kuwezesha huduma hiyo.
Chuo
hicho ni miongoni mwa Shule na Vyuo vingine kadhaa ambavyo vipo katika
hatua za mwisho za mazungumzo na Vodacom ya kuviwezesha kutumia huduma
ya M-pesa katika ulipaji wa karo ada nynegine katiika taasiis hizo za
elimu nchini.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo eneo la Kipawa kilipo chuo hicho Dar
es Salaam, Mkuu wa Ukuzaji Biashara; M-Pesa Jackson Kiswaga amesema
kuanza kwa huduma hiyo ni mwendelezo wa azima ya Vodacom ya kuyaleta
maisha ya watanzania kiganjani kupitia teknolojia ya simu za mkononi.
Amesema
katika mipango ya kuwezesha malipo ya karo kwa M-pesa Vodacom imeanza na
VETA kipawa kinachotoa elimu zaidi ya masula ya teknolojia ingawa
mipango ni kufikisha huduma hiyo kwa vyuo vyote vya VETA nchini pamoja
na vyuo vingine na shule.
"Tunajivunia
ushirikiano huu unaoleta mapinduzi mengine ya kiteknolojia na kimfumo
wa jinsi tunavyoendesha biashara zetu na hata maisha yetu, na ni
matarajio ya Vodacom kwmaba huduma hii itakuwa na mafanikio makubwa
katika kukidhi mahitaji ya wanachuo.” anasema Kiswaga.
Aidha,
Kiswaga anaeleza kuwa ushirikiano huo utatoa njia mbadala katika malipo
ya ada, na kusisitiza kuwa huduma ya M-Pesa ni salama, haraka na ya
uhakika, kwa kuwa imeleta mapinduzi katika huduma mbalimbali za kifedha
tangu kuanzishwa kwake miaka minne iliyopita.
Kwa
upande wake, Mkuu wa chuo hicho, Lucius Luteganya, amesema uongozi na
jumuiya nzima ya chuo cha Veta Kipawa wameupokea mfumo wa huduma hiyo
katika mtazamo chanya, kwa kuzingatia hali halisi ya muktadha wa
teknolojia ya sasa na vipaumbele vyake.
"Ukweli
wanafunzi walio wengi wanapopewa fedha za karo na wazazi wao
hawazifikishi na hata wakizifikisha zinafika zikiwa pungufu, sasa
kupitia huduma ya M-Pesa wazazi watapata fursa ya kulipa ada moja moja
wakiwa nyumbani, na kupiga simu kuthibitisha badala ya kuwapatia
wanafunzi mikononi." anasema Luteganya.
Amesema
suala la wanafunzi kupanga foleni au kuchukua muda mrefu wakati wa
ulipaji wa karo sasa limepatiwa ufumbuzi, kwani adha hiyo imekuwa
ikizorotesha shughuli nyengine chuoni hapo hasa kwa idara zinazohusika
na malipo, kuwapotezea muda mwingi wananfunzi na kujikuta wakichelewa
vipindi darasani na hivyo kupunguza ufanisi wao kimasomo.
Aidha,
Luteganya anasema pamoja na mambo mengine, vyuo vya Veta nchini ni wadau
wakubwa wa masuala ya teknohama, hivyo wanaona fahari kuwa mfano wa
kuigwa kwa wao kuwa sehemu ya teknolojia zenye manufaa zinazoibuliwa
ndani ya jamii za kitaifa na kimataifa.
Huduma ya
M-Pesa ya Vodacom Tanzania ina mawakala zaidi ya elfu 40,000 nchini
kote, na ni pekee ambayo inaongoza kwa kuwa na wabia wengi w akibishara
katika kila Nyanja na hivyo kutoa wigo mpana zaidi wa wananchi kunfaika
nayo katika kulipia huduma mbalimbali pamoja na kuhifadhi, kutuma na
kupokea fedha.
Kupitia
M-pesa mteja wa Vodacom anaweza kulipia tiketi za ndege, huduma za maji,
umeme na ving’amuzi, kulipia manunuzi ya bidhaa katika baadhi ya maduka
makubwa – Super Markets, kulipia bima, kulipia michango katika baadhi
ya mifuko ya hifadhi ya jamii na sasa karo katika chuo cha VETA kipawa.