Joseph Ngilisho,Arusha
MFUGAJI Ngeresa Ole Metemi (55) mkazi wa Olkokola wilayani
Arumeru,ambaye hivi karibuni alitoa malalamiko kwa kumtuhumu
mwekezaji,Calleb Simonson wa shamba la maua, raia wa Marekani,pamoja
na polisi wilayani humo, kumbambikia kesi ya jinai,sasa amedai
kutishiwa kuuawa kwa kukatwa kichwa na kuchomewa boma lake na
wanakijiji wenzake.
Kwa mujibu wa taarifa aliyoiandika kwenda kwa mkuu wa wilaya ya
Arumeru na idara mbalimbali za usalama,Ngereza anamtuhumu mwenyekiti
wa kitongoji cha kanda ya Sikiret,Peter Lesukui kuwa ni ndiye
aliyeongoza kikao cha wanakijiji ambao walitoa kauri ya yeye kusakwa
na kukatwa kichwa.
Pia amewatuhumu wazee wa ukoo wakiongozwa na Lemali Sembeo pamoja
Ngotee Lisilale kuwa ni wachochezi wanaotaka kuhatarisha maisha yake.
Mfugaji huyo anadai kwamba mnamo januari 3 mwaka huu,aliwakamata
wafanyakazi wanne wa mwekezaji huyo na kuwafikisha mahakamani
,wakikabiliwa na shitaka la wizi wa ng’ombe wake watatu ,wenye thamani
ya shilingi milioni 4.
Alisema kufuatia kukamatwa kwa wafanyakazi hao na kufikishwa
mahakamani,baadhi ya wanakijiji wakiwemo wanandugu wa washtakiwa hao
wakishirikiana na mwekezaji huyo,wamekuwa wakiendesha vikao vya mara
kwa mara vya kutaka kumdhulu mfugaji huyo baada ya kuchukizwa na hatua
ya kukamatwa kwa wenzao.
Kwa mujibu wa Ngeresa kikao kilichofanyika januari 14 kijijini hapo na
vingine vya nyume vinaratibiwa na mwekezaji huyo kwa kuwatumia baadhi
ya wanakijiji na viongozi wa mila.
Hata hivyo alibainisha kwamba katika kikao hicho wanakijiji
walikubalina kukutana siku ya jumatatu,januari 21 kwa ajili ya
kukubaliana kwa pamoja kutekeleza mpango huo wa kumdhulu kwa kumkata
kichwa na kumchomea makazi yake(boma).
Awali Ngeresa akisimulia zaidi alisema, mnamo tarehe 27/6/2011 ng’ombe
wake watatu wa maziwa walikamatwa na wafanyakazi wa mwekezaji Simonson
wakidaiwa kupita karibu na shamba hilo la maua kitendo ambacho
kilimlazimu kufuatilia na kutakiwa kulipa faini ya shilingi 60,000 ili
akabidhiwe ng’ombe wake.
Alisema aliamua kulipa kiwango hicho cha fedha ili achukua ng’ombe
wake na kupatiwa risiti , hata hivyo alishangaa kuona mwekezaji huyo
kutomrejeshea mifugo yake na badala yake amekuwa akipigwa danadana
,hali iliyomlazimu kwenda kutoa taarifa kituo hicho cha polisi Usa
River ili kupata msaada zaidi.
Anaeleza kuwa, akiwa na matumaini ya kusaidiwa kituoni hapo,ili apate
mifugo yake ,ghafla mambo yaligeuka na kuwa kinyume na matarajio,
kwani msaada alioutarajia ukawa shubini akajikuta akigeuziwa kibao na
kukamatwa huku akielezwa kuwa ametenda kosa la unyang’anyi wa mbwa wa
mzungu kwa kutumkia silaha.
‘’kwakweli nilikamatwa na kupelekwa magereza nimekaa huko kwa muda wa
miezi saba kwani kesi niliyofunguliwa haikuwa na mdhamana hadi kesi
yangu iliposomwa mahakamani na mahakama iliifuta na kuniachia huru
kutokana na walalamikaji kuonekana walitoa ushahidi wa uwongo
’’alisema Ngeresa.
Ngeressa anamtuhumu aliyekuwa mkuu wa polisi wilayani humo William
Nyambuga ambaye sasa amehamishiwa mkoani Mara kuwa alijenga mahusiano
ya karibu na mwekezaji huyo kwani mara kwa mara amekuwa wakimbambikia
kesi mbalimbali kutumia vituo hivyo vya polisi Oldonyo Sambu na
Usariver ambavyo vipo chini yake kwa lengo la kumdhoofisha asiendelee
kudai ng’ombe wake.
Alisema baada ya kuachiwa huru na mahakama,aliamua kupeleka malalamiko
yake kwa aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa wa Arusha,Thobias Andengenye
ambaye baada ya kumweleza alimtaka afungue kesi ya wizi wa
mifugo,ambapo upelelezi ulianza kufanyika upya.
Alisema baada ya upelelezi kufanyika , polisi ilibaini kwamba ng’ombe
hao walichukuliwa na mwekezaji huyo kwa kuwatumia wafanyakazi wake
ambapo mapema mwaka huu,polisi mjini hapa iliwatia mbaroni wafanyakazi
wanne wa mzungu huyo na kuwafikisha mahakama ya wilaya .
Hata hivyo Ngeressa ameshangaa kutomwona mwekezaji huyo akishindwa
kukamatwa na kuunganishwa na wafanyakazi wake kwani kwa mujibu wa
maelezo yake anasema kwamba Simonson ni mshtakiwa namba moja katika
kesi hiyo inayosikilizwa katika mahakama ya wilaya ya Arumeru.
‘Kwa kweli mimi ninasikia uchungu sana kwani mhusika mkuu katika
shitaka hili hajatajwa nkabisa wakati mzungu huyo ndiye
ninayemlalamikia katika kesi yangu angetakiwa awe ndo mshtakiwa namba
moja halafu wengine ndo wafuate sasa kilichofanyika mimi nashindwa
kuelewa naomba haki itendeke jamani.’alisema Ngeresa.
Mfugaji huyo anamshukuru sana aliyekuwa mkuu wa polisi mwaka jana
Thobias Andengenye pamoja na RCO Wambura ambao kwa kiwango kikubwa
walibaini uovu wa polisi wao ukiwemo uovu wa aliyekuwa mkuu wa polisi
wilayani Arumeru,Williamu Nyambuga ambaye alishiriki kumbambikia kesi
nyingi za jinai chini ya shinikizo la mwekezaji.
Washtakiwa waliotiwa mbaroni na kufikishwa mahakamani ni Yona
Melao(30),Mathayo Alphayo (34),Philpo Saitoti(26) na Mitishili
Kotishoni(26) wote wafanyakazi wa mwekezaji huyo na wakazi wa Olkokola
wilayani Arumeru .
Kwa upande wa m kuu wa polisi wilaya ya Arumeru Benedikti Mpujilwa
alikiri kupokea barua ya malalamiko ya mfugaji huyo na kuahidi
kuifanyia kazi .