YANGA WAREJEA KESHO DAR ES SALAAM



Kikosi cha wachezaji wa Young Africans na viongozi wake wakiwa mbele ya hotel ya Fame Residence - Antalya Uturuki
Timu ya Young Africans iliyokuwa imeweka kambi ya mafunzo kwa muda wa wiki mbili inatarajiwa kuondoka majra ya mchana mjini Antalya - Uturuki kupitia Istambul ambapo inatarajiwa kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa JNIA Dar es salaam majira ya saa 10 kasorobo kwa saa za Afrika Mashariki.
 
Young Africans ambao ni Mabingwa mara 23 wa Ligi Kuu ya Tanzania bara na Bingwa mara tano (5) wa kombe Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati iliweka kambi ya mafunzo katika mji wa Antalya kwa muda wa takribani siku 14 ambapo ilikuwa ikifanya mazoezi na kupata fursa ya kucheza michezo mitau (3) ya kirafiki.
 
Katika kambi yake ya wiki mbili Young Africans iliapata fursa ya kucheza michezo mitatu ya kirafiki na timu za   Arminia Bielefeld ya ligi daraja la tatu Ujerumani, Dinzlispor FC ilyopo ligi daraja la kwanza nchini Uturuki na Emmen FC iliyopo ligi daraja la kwanza nchini Uholanzai.
 
Akiongelea michezo ya kirafiki mitatu waliocheza na timu za Armini Bielefeld, Deinizlispor na Emmen Fc kocha mkuu wa Yanga Ernest Brandts amesema michezo ilikuwa ni mizuri na wamepata nafasi ya kuona mapungufu machache yaliyojitokeza na anaamini watayafanyia kazi na kuendelea kufanya vizuri.
 
Tumecheza michezo mitatu, wa kwanza tulitoka sare na Amrinia Bielefeleld, mchezo ulikua mzuri na timu yangu ilicheza vizuri kwa dakika 90 zote za  mchezo licha ya Arminia kusawaisha bao dakika za lala salama huku mwamuzi aklishindwa kutoa maamuzi sawa na mshika kibendera wake, ambapo mfungaji alikua maeotea.
 
Mchezo wa pili dhidi ya Denizlispor nao pia timu ilicheza vizuri na kuweza kutengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini umakini wa washambuliaji ulitukosesha ushindi kwani Tegete alitumia nafasi aliyoipta kufunga bao la mapema kabla ya Waturuki hawajasawazisha kwa bao la utata  kisha kupewa penati ya utata pia.
 
Mchezo wa mwisho dhidi ya Emmen FC ulikuwa mzuri pia na kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza tuliutawala mchezo na kupata nafasi kadhaa za kufunga mabao lakini kutokua makini wa washambuliaji wetu pia kulichangia sisi kukosa ushindi, kabla ya kipindi cha pili Emmen FC kucharuka na kupata mabo mawili ya haraka haraka kutokana na uzembe wa walinzi na mlinda mlango Yusuph abDUL
 
Tunaushukuru uongozi kwa kukubali kutupa nafasi ya kuweka kambi Uturuki, tumkeaa pamoja kwa mda mrefu huku tukitoka mafunzo kwa vitendo, vifaa na mahitaji yote vikiwepo ,kukiwa na hali ya utulivu, kifupi tumejifunza mambomengi sana ya msingi ambayo yatatusaidia kufanya vizuri katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom na mashindano ya kimataifa yatakayotukabili alisema 'Brandts'
 
Timu itaondoka  Antalya majira ya saa  9:30 mchana na kufika katika mji wa Instabul majira ya saa  10:50 jioni , kisha baadae majira ya saa 1 na robo usiku itaanza safari ya kuelekea Dar es es salaam ambapo inatazamiwa kufika uwanja wa ndege wa kimataifa  JNIA jumatatu majira ya saa 10 kasoro alfajiri.
 
Msafara utakua na jumla ya watu 33, wachezaji 27, na viongozi 6
 

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post