MKUU WA WILAYA YA ARUSHA AELEZA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI KWA KIPINDI CHA MWAKA 2005-2012

 Mkuu wa wilaya ya arusha akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na utekelezaji wa ilayani ya uchaguzi kwa kipindi cha mwaka 2005-2012

 picha ya juu na chini ni baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Arusha  wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Arusha John Mongela wakati akielezea mafanikio ya utekelezaji wa ilani ya chama katika manispaa ya Arusha tangu mwaka 2005-2015
 Na Woinde Shizza,Arusha
Imeelezwa kuwa ilani ya ccm kwa miaka saba katika wilaya ya arusha imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika njanja zote zikiwemo sector ya elimu ,afya,mazingira,na miundombinu ikiwemo mji wa arusha kuwa jiji rasmi.

Hayo yameelezwa na mkuu wa ilaya ya Arusha John Mogella mbele ya waandishi wa habari wakati akitoa taarifa hiyo katika hotel ya palace hapa jijini arusha  na kusema kuwa sector zote zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani toka mwaka 2005 hadi mwaka 2012 karibu utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi imetekelezwa.

Bw Mogella amesema katika sector ya elimu amesema wamejenga madarasa 172,matundu ya vyoo 225,ambapo shule za msingi zimeongezeka 70 ambapo kwa shule za sekondari zimeongezeka 23ambapo awali zilikuwa saba ,ambapo walimu na vifaa vya usimamizi wameongezeka 534 kwa miaka hiyo saba pamoja na idadi ya vyuo vya shahada ya juu vikuu kupandishwa hadhi  na kufikia 8 .

Amesema kwa upande wa afya mkuu mogela amesema kuwa wameweza kuboresha huduma ya mama na mtoto ambapo vituo 5 na zahanati 68 zimeboreshwa kwa uhakika wa upatikanaji wa dawa na huduma bora,huku akifafanua kuwa wameipandisha hadhi kituo cha afya cha kanisa st.elizabert na kuwa hospitali ya wilaya huku akisema kuwa katika hospitali hilo kuna kituo kikuu kitakachotoa huduma kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi ambapo kitatoa huduma bure.

Kwa upande wa miundo mbinu amesema kuwa barabara nyingi zimejengwa katika kiwango cha lami katika barabara hasa za katikati ya mji ambapo hadi sasa barabara 23 zenye urefu wa km 8 zimekamilika ambapo mkradi huu unaofaziliwa na benki ya dunia kwa kiasi cha dola million 7 za kimarekani,ambapo ni awamu ya kwanza na awamu ya pili itajenga barabara ya njiro,kanali ndomba,pamoja na kujenga dampo la kisasa la kisasa,yakiwemo ujenzi wa madaraja 9 katika wilaya ya arusha.

Mogela akiongezea kuhusu upande wa maringira hasa upande wa maji amesema asilimia 83 ya wakazi wanaoishi katika jiji la arusha wanapata maji safi na salama tofauti na awali ilikuwa ni asilimia 42 tu ya wakazi ndio waliopata huduma hiyo ya maji salama ,ambapo amesema kuwa wanamkakati wa mradi wa ujenzi wa miundo mbinu utakao gharimu shilingi million moja.

Katika swala la mazingira amesema wamepiga hatua kwani wameweza kulinda vyanzo vya maji kwa kushirikiana na AUWSA ikiwemo misitu,kuzuia uoshaji wa magari pembezoni mwa mito,na kuzuia ukataji wa miti katika misitu iliyopo ndani ya jiji ikiwemo kuboresha usafi ndani ya jiji letu.

Aidha alisema pamoja na mafanikio hayo pia kuna changamoto zinzoikabili jiji hili ikiwemo ya kusafisha hati chafu ya jiji hili ,ambapo baadhi ya viongozi wabadhirifu wa raslimali wamewajibishwa kutokana na makosa yao ikiwemo kufikishwa mahakamani paoja na kufukuzwa kazi.
Pia aliongezea kuwa changamoto nyingine ni demokrasia ambapo wilaya yetu ina viongozi wa vya  vya siasa tofautitofauti ambapo alitolea mfano mbunge wa chadema katika jimbo la mjini arusha kutofautiana katika utekelezaji na uwajibikaji katika kuwatumikia wananchi wa wilaya hii .

Mwisho mkuu wa wilaya ya arusha Mogella alitoa wito kwa wakazi wa jiji la arusha kuendelea kushirikiana na viongozi katika kuhakikisha hali ya jiji inakuwa tulivu ambapo kwa kiasi kikubwa katika swala la ulinzi na usalama ikiwemo dhana ya ulinzi shirikishi na tii sheria bila shuruti.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post