UN YAENDESHA MAFUNZO KUHUSU SHUGHULI ZA UNDAP NA HAKI ZA BINADAMU KWA WAANDISHI WA HABARI VISIWANI ZANZIBAR



Afisa habari ngazi ya Taifa wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi.Usia Ledama akieleza nia ya Umoja wa Mataifa Tanzania kuendesha mafunzo kwa waandishi wa habari wa Visiwani Zanzibar juu ya Haki za binadamu na jinsi Mpango wa msaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDAP) unavyoshirikiana na Serikali ya Zanzibar katika maeneo matatu muhimu ambayo ni Uchumi, Kupunguza umaskini na Utawala na uwajibikaji. Semina hiyo imefanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View visiwani Zanzibar.
Mratibu wa FAO Ofisi ya Zanzibar Ali Haji Ramadhan akitoa hotuba ya makaribisho katika mkutano na waandishi wa habari wa Visiwani Zanzibar ambapo amesema wanatarajia kupata mawazo mengi zaidi ya kujenga kutoka kwa waandishi ambapo yatasaidia Umoja wa Mataifa pamoja na Serikali kuihudumia nchi kwa upeo wa juu zaidi.
Mwakilishi wa mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa Zanzibar Anna Senga akizungumza na waandishi wa habari wa visiwani Zanzibar kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo wao kama UN katika kutekeleza hoja za mipango wa maendeleo (UNDAP) kutokana na kuchelewa kupewa majibu na uchelewashaji wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo.
Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mafunzo hayo ambapo ameelezea Mpango Mkakati wa UNDAP visiwani Zanzibar ikiwemo kutoka ufafanuzi wa mafanikio pamoja na changamoto zinazoukabili mpango huo.Amesema mpango huu ni wa pamoja kwa ajili ya Tanzania unaendena na mafanikio ya malengo ya maendeleo ya kimataifa ambapo unachukua nafasi ya program za pamoja na miradi mingi inayodhaminiwa na UN chini ya Model ya misaada ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa kwa mpango wa kazi moja ulioshikamana kwa ajili ya mifuko ya fedha, program na wakala zote za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo hayo ya siku moja wakimsikiliza Afisa Mawasilano wa Umoja wa Mataifa nchini Hoyce Temu.
Katibu wa Chama cha wanasheria wanawake Zanzibar Hamisa Mmanga Makame akitoa somo katika mafunzo hayo ambapo amezungumzia masuala ya Haki za Binadamu, umuhimu wa kuzingatia jinsia na wajibu wa vyombo vya habari katika kuleta usawa.
Afisa Mipango mwandamizi wa shirika la kazi duniani (ILO) Anthony Rutabanzibwa ambapo amevipongeza vyombo vya habari vya Afrika Mashariki kwa kutoa kipaumbele katika habari zinazohusu haki za binadamu na kuwataka waandishi kuzingatia zaidi habari za kiuchunguzi ili kuwa na uhakika zaidi na yale wanayoaandika ikwemo kujua chanzo cha habari unayoitoa.
Mwenyekiti wa UNCG Yusuph Al Amin akielezea mada ya umuhimu wa mawasiliano kwa maendeleo na kuwataka wamiliki wa vyombo vya habari na serikali kwa ujumla kubadilisha sera zinazosimamia vyombo hiyo ili ziweze kutoa fursa kwa waandishi kuwa huru katika uandishi na kuripoti habari bila kubanwa.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Zanzibar Hassan Khatibu, Mratibu wa FAO Ofisi ya Zanzibar Ali Haji Ramadhan, Mwakilishi wa mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa Zanzibar Anna Senga, Mwezeshaji wa mafunzo hayo mwandishi mkongwe Salim Said Salim na Mwenyekiti wa UNCG Yusuph Al Amin.
Rais wa Umoja wa vilabu vya waandishi wa habari Kenneth Simbaya akitoa maoni yake kuhusiana na nini kifanyike katika kuboresha tasnia ya habari ambapo ameshauri mafunzo kuendelea kutolewa si tu kwa waandishi pia kwa wamiliki wa vyombo vya habari.
Pichani Juu na chini ni baadhi ya waandishi ws habari wa visiwani Zanzibar wakichangia mawazo yao wakati wa mafunzo hayo.
Afisa mipango wa Baraza la Habari Tanzania Ofisi ya Zanzibar Shifaa Said Hassan akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo.
Sehemu ya waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo ya siku yaliyoendeshwa na Umoja wa Mataifa visiwani Zanzibar.
Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akijadili jambo na wafanyakazi wenzake wakati wa mafunzo hayo

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post