Bluestar kuitambulisha singo yake mpya


MSANII wa mjini Arusha anayekuja kwa kasi katika mziki wa kizazi kipya
hapa nchini Hamisi Omari(20)maarufu kama Bluestar anatarajia kuachia
singo yake ya tatu inayokwenda kwa jina la Tunachafua.

Akizungumza na gazeti hili amesema kuwa singo hiyo ambaye
amemshirikisha Mr Blue na Swaga Boy na kurekodiwa katika studio ya
Danlumark kwa Macko P ya jijini Dar es Salaam itaanza kusikika rasmi
wiki hii katika vituo mbalimbali vya redio na kutazamwa katika
luninga.

“Nawataka wapenzi wa muziki wa kizazi kipya na mashabiki wangu kwa
ujumla wakae mkao wa kula kupokea wimbo huo kwani ni moto wa kuotea
mbali”alisema Bluestar.

Amezitaja nyimbo zake mbali ambazo tayari aliishazitoa mwaka jana kuwa
ni Digidagi aliyemshirikisha Chris G ambayo ameirekodia katika studio
ya Fnock kwa Sumtimber na Njoo aliyeirekodia katika studio ya
Dunlumark.

Msaanii huyo ambaye alianza muziki mwaka jana amesema kuwa matarajio
yake ni kuja kuwa mwanamuziki maarufu sana ndani na nje ya nchi na
kwamba katikati ya mwaka huu atatoa albamu yake ya kwanza na kutoa
wito kwa mashabiki kumuunga mkono.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post