Afrika
Kusini na Tanzania zimekataa kuhusika katika sherehe ya makubaliano ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Nchi hizi zinasema kuwa hazikuarifiwa
juu ya jambo hili na hivyo hazitaki kuwa chanzo cha mvutano kandani.
Lakini
waziri wa usalama wa Afrika kusini , anasema kuwa kwa mashangao wao
walipowasili jijini Addis Ababa, Ethiopia kwa ajili ya mkutano wa umoja
wa Afrika walipata barua ambayo ilisema kuwa Afrika kusini ilikuwa
imekubali kuwa ingekuwa kati ya nchi washahidi wa mipango ambayo
inatafuta sulushu nchini Kongo. Waziri wa Usalama Nosiviwe Mapisa
anaelezea:
“Hii
ilitushangaza kwani hiyo si aina ya mkataba amabyo nchi yeyote inaweza
kujihusisha nayo kwa urahisi, kunafaa kuwe na mikutano na majadialiano
kwa undani kati yetu kuhakikisha kuwa tuaelewa tunayojihusisha nayo.
Labda mkataba amabyo imetengeneza tayari haina shida lakini jinsi jambo
hili limejitokeza si mzuri, inaweza kuleta shida sana kati ya nchi
zetu.”
Kulingana
na hati ambayo ilikuwa tayari imetayarishwa kuhusu swala la Kongo nchi
za kutoka jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa Afrika, Angola, Afrika
Kusini na Tanzania ndizo zingetarajiwa kuwa washahidi kuhusika katika
sherehe ya kutia saini makubaliano ya Kongo. Nosiviwe Mapisa waziri wa
usalama wa Afrika kusini anaelezea tena.
“Swali
letu ni, kwa nini nchi zingine hazijahusihwa? Kwasababu tumekuwa
tukijaribu kutatua swala la Kongo tukiwa nchi 14, kwa hivyo sisi
kukubali kuhusika pekee yetu katika shere hii ingefanya kuwe na mvutano
usiofaa.”
Tanzania
na Afrika Kusini zimedhihirisha kwamba zitahusika kutia saini tu katika
makubaliana kuhusu Kongo ambayo itahusisha nchi zote zilizohusika
katika kutafuta suluhu kwa Kongo yaani nchi wanachama wa maziwa makuu na
nchi zote za jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa Afrika.