Wananchi wa
kata ya mbuguni wamempongeza mbunge wao wa jimbo la arumeru mashariki Joshua Nasari
kwa kutimiza ahadi ya kurejesha soko la mbuguni lilisimamishwa kufanya kazi kwa
muda wa miaka ipatayo 10 ikiwa ni kupisha ujenzi wa stendi ya magari katika soko hilo .
Wanachi hao
ambao ni wafanyabiashara wa soko hilo la Mbuguni wakati wakizungumza na Redio
hii walisema kuwa wanampongeza mbunge
wao kwa kufikia hatua nzuri ya kurejesha soko hilo kwani wamekua katika wakati
mgumu kwani walichukua mikopo ya biashara lakini toka mwaka 2003 akuna biashara
waliofanya baada ya kusimamishwa kufanya biashara hiyo na kupisha ujenzi wa
stendi ya mabasi .
Mmojawapo wa
mfanyabiashara wa zamani kutoka katika soko hilo la Mbuguni Bi Grace Kaaya alielezea kuwa ujio wa soko
hilo umewasaidia sana ijapokuwa kwa sasa hivi wanakabiliwa na hali ngumu ya
kutokuwa na mitaji ya kuanza biashara mpya.
“Unasikia
ndugu mwandishi tunamshukuru sana mheshimiwa mbunge kwa kuwa wakati soko hili
linafungwa tulikuwa tunauwezo wa kusomesha watoto wetu na sasa tukashindwa kwa
hali hii tunatarajiwa tutaweza kuwalipia ada watoto wetu”, Alibainisha Bi
Grace.
Pamoja na
kuona kuwa ujio wa soko hilo unaleta nafuu pia alitoa rai kwa Halimashauri ya
Wilaya ya Arumeru pamoja na Mbunge kuakikisha kuwa wanaboresha hali ya miundo
mbinu ya soko hilo ili kuwawaezesha kufanya biashara zao kiufanisi zaidi.
Naye katibu
wa mbunge wa Arumeru Mashariki Bwana
Totinani Ndone alisema kuwa kwa mujibu
wa sheria za serikali za mitaa amabapo inaeleza kuwa Halimashauri
endapo inataka kufanya mswala ya Maendeleo ni
shuruti kuwajulisha wakazi husika
na kukubaliana na sio kujichukulia uwamuzi pasipo kufikia makubaliano.
Ambapo alitoa
rai kubwa kwa uongozi wa Halimashauri ya Wilaya ya Arumeru kuhakiksha kuwa
wakazi wa Wilaya hiyo wanayo Moyo mkubwa wa kushirikiana nao hivyo ni budi
kushirikiana nao kwa upana mkubwa ili kuiletea maendeleo katika halimashauri
hiyo ya Arumeru.
Wakati
huo huo Mkurugenzi wa Wilaya Arumeru
bwana Transes Kagenzi alipozungumza na
gazeti hili alisema kuwa halimashauri
yake imetenga jumla ya shilingi milioni 50
kwa ajili ya ukarabati wa soko hilo sambamba na kuangalia jinsi gani ya kutatua
miundo mbinu chakavu ya soko hilo ikiwemo tatizo la maji pamoja na huduma ya
vyoo.