Ticker

6/recent/ticker-posts

WATAKIWA KUJENGA UMOJA NA MSHIKAMANO

Viongozi wa madhehebu mbali mbali ya dini wametakiwa kudumisha umoja na mshikamano sanjari na kuacha kudharaulina kwani hilo litaleta kumong’onyoka kwa maadili na kubomoa amani yetu na badala yake kuhubiri ushirikiano na kuwajenga waumini wao kuwa na hofu ya mungu.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu mkuu wa ccm ndugu Abdurahaman Kinana kwenye maadhimisho ya siku ya kumbu kumbu imamu Husein yanayoadhimishwa na dhehebu la khoja Ithnasher kote duniani na kufanyika kwenye msikiti wa jamii hiyo jijini hapa juzi.

Kinana alisema kuwa hivi sasa jamii ya watanzania imeingia kwa baadhi ya watanzania kuwauza wenzao huku ni kutaka kuleta mpasuko kiimani na wengine kujenga uadui kwa kudharau madhehebu za wenzao tufike mahali tuheshimu na kujifunza yale yalio kwa mwenzako kwa ustaarabu na kuvumiliana.

“Ustaarabu wa kuvumiliana na kuweka upendo miongoni mwetu ndiyo silaha ya kuitunza amani iliyopo hapa nchini nawaombeni viongozi wa dini hapa nchini kuwajenga waumini kuwa na hofu ya Mungu ili taifa letu lisikumbwe na mipasuko ya kiimani”alisema Kinana

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo Mkuu wa wilaya ya Monduli Jowika Kasunga alisema kuwa kumekuwa na vikundi vya kiimani ambavyo vimesajiliwa lakini vimekuwa vikichochea uvunjifu wa amani na kuvitaka kuacha kuipoteza amani iliyopo kwani kutafuta ni gharama kuliko kuitunza
Kasunga alisema kuwa anatoa wito kwa viongozi wa madhebu hapa nchini kuwajengea hofu ya Mungu watumishi wa serekali na wananchi ilituishi salama kwa amani iliyopo serekali pekee haiwezi kuitunza bila ya kushirikiana nanyi na watanzania.

Nae Sheikh wa mkoa wa Arusha Shaban bin Simba alisema kuwa nchi kuingia kwenye machafuko ni jamii kumuasi muumba wao na kutokuwa na hofu ya siku ya malipo na kuwataka viongozi wa dini kujenga ushirikiano wa karibu na maskizano

Post a Comment

0 Comments