Timu ya Real Madrid
imezidi kuingia kwenye presha kubwa ya kusakamwa na Mashabiki baada ya
jana kushindwa kuifunga Osasuna ambayo ni moja ya Timu 3 zilizo mkiani
baada ya kutoka sare 0-0 katika Mechi ya La Liga iliyozidi
kuwathibitishia kuwa Msimu huu Ubingwa umewatoka.
Usiku wa jana ulikuwa wa balaa kwa Real
Madrid ambao walicheza bila Nyota wao, Cristiano Ronaldo na Sergio
Ramos, ambao wanatumikia Kifungo, nae Mchezaji wao Kaka, alieanzia
Benchi, alidumu Dakika 19 tu Uwanjani na kutolewa nje kwa KadiNyekundu
baada ya kupata Kadi za Njano mbili na Bao lao safi lililofungwa na
Jose Maria Callejon kukataliwa kwa Ofsaidi ya utata.Matokeo hayo
yamewafanya Real Madrid wawe Pointi 4 nyuma ya Atletico Madrid, walio
nafasi ya pili, na Pointi 15 nyuma ya Vinara Barcelona.Barcelona na
Atletico Madrid wanaweza kuzidisha mapengo yao hayo hivi leo baada ya
Mechi zao.
Jose Callejon akijaribu kumfunga kipa wa Osasuna
Sami Khedira (katikati) akikwaruzana na wachezaji hapa na timu yake ikiambulia droo ya 0-0
RATIBA/MATOKEO:
LA LIGA
Jumamosi Januari 12
Real Valladolid 3 Real Mallorca 1
RCD Espanyol 1 Celta de Vigo 0
Osasuna 0 Real Madrid 0
Valencia 2 Sevilla FC 0
Jumapili Januari 13
Real Betis v Levante
Real Sociedad v Deportivo La Coruna
Atletico de Madrid v Real Zaragoza
Malaga CF v FC Barcelona