Kundi la Scorpion Girls likiongozwa na Isabela Mpanda (katikati) likiporomosha burudani wakati wa Tamasha la Usiku wa Mastaa wa Filamu lililofanyika Dar Live usiku wa kuamkia leo.
Bendi ya Twanga Pepeta ikitoa burudani katika Tamasha la Usiku wa Mastaa wa Filamu lililofanyika Dar Live usiku wa kuamkia leo.
Tamasha
la Usiku wa Mastaa wa Filamu lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika
Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar
es Salaam limeacha historia baada ya kutawaliwa na burudani za kila
aina kutoka kwa wasanii wa filamu na wale wa Bongo Fleva. Pichani juu ni
baadhi ya matukio yaliyochukua nafasi wakati wa tamasha hilo.
(PICHA ZOTE: ERICK EVARIST NA MUSA MATEJA/GPL)