LOWASA AMSIFU RAIS KIKWETE KWA KUMALIZA TATIZO LA MAJI MONDULI

 

Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa amezindua mradi wa maji wa Bwawa la Leken katika Kijiji cha Selela uliogharimu Sh1.1 bilioni, huku akiupongeza uongozi wa Rais Jayaka Kikwete kwa kusaidia kuondoa tatizo hilo kwa binadamu na mifugo wilayani hapa.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mradi huo juzi, Lowassa, ambaye ni mbunge wa jimbo hilo tangu mwaka 1995, alisema chini ya uongozi wa Rais Kikwete, Monduli imepata manufaa makubwa na akawataka wakazi wa jimbo hilo kumpongeza.
Lowassa alisema alipochaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa mbunge jimboni hapa, changamoto aliyoikuta ilikuwa ni ya maji ambayo kwa sasa imepungua baada ya upatikanaji wa maji kufikia asilimia 60.
Akizungumzia mradi wa bwawa hilo alisema unatarajiwa kunufaisha kata zaidi ya tano kutokana na bwawa hilo kuwa na uwezo wa kuhifadhi lita 392.04 milioni za ujazo milioni katika kipindi cha miaka mitatu hata kama mvua hazitanyesha.
Alisema kukamilika bwawa hilo ni sehemu ya mipango ya Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Kitengo cha Maafa waliotoa Sh3 bilioni .
Mkuu wa wilaya hiyo, Jowika Kasunga alisema kukamilika kwa bwawa hilo ni utekelezaji wa mipango ya Serikali wa kuondoa tatizo la maji kwa binadamu na mifugo.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia