mkuu wa wilaya ya Hai Novatus Makunga akiwa anasalimiana na wachezaji wa timu Mango Garden ya jijini Dar es salaam wakati walivyokuja kushiriki bonanza la kitambi noma lililofanyika katika kiwanja cha kumbukumbu ya sheikh Amri Abeid ya jijini Arusha
katika bonanza hili la kitambi noma kuliuzuriwa na watu wengi akiwemo mmbunge wa jimbo Meatu kupitia CHADEMA Aliyevaa tisheti ya blue
Mh. Meshack Opulukwa
kulikuwepo pia na mashindano ya kukimbia na magunia ambapo katika mashindano haya mchezaji kutoka timu ya Mango Garden alishinda
washabiki wa timu ya kitambi noma ya jijini Arusha wakishabikia ushindi mara baada ya kushinda kukimbiza kuku
wachezaji w timu ya Benson kampani wakivuta kamba
wadau wa timu ya kitambii noma wakiwa pamoja na mdada wa libeneke la kaskazini katika bonanza la kitambi noma siku ya pasaka
muheshimiwa mkuu wa wilaya ya Hai Novatus Makunga akiwa na mdada wa libeneke la kaskazini(woinde shizza Blog) wakati wa bonanza la pasaka lililoaadaliwa na timu ya kitambi noma ya jijini Arusha ambapo mkuu wa wilaya ni mwanachama wa klabu hiyo
mambo ya nyama choma nayo yalikuwepo
KITAMBI noma
mabingwa wa jumla wa bonanza la pasaka lililofanyika katika uwanja wa
kumbukumbu ya sheikh Amri Kaluta Abeid huku timu ya Mango Garden ya Kinondoni
ikishika nafasi ya pili ikiwa ni katika kusherehekea sikukuu ya pasaka kwa
michezo mbalimbali.
Bonanza hilo
lililoandaliwa na Klabu ya Kitambi noma yenye maskani yake jijini hapa na
kufadhiliwa na kampuni ya bia (TBL)liliwakusanya mamia ya wapenda michezo na
kushudia michezo ya kukimbiza kuku,kukimbia na magunia,soka,Kunywa bia,kuvuta
kamba na burudani ya muziki kwa siku nzima ya pasaka.
Akifungua
bonanza hilo Mkuu wa wilaya ya Hai Novatus Makunga al;iwataka washiriki wa
bonanza hilo kufahamu kuwa michezo ni afya na burudani na tunatarajia kuona
burudani kutoka kwenu kwani pia nimefarijika kuwaona marafiki zangu ambao
wengine walikuwa wakicheza ligi kuu lakini kwa sasa vitambi vimewanyemelea
hivyo michezo ni fursa nzuri ya kuvipunguza.
Makunga
akawaka washiriki na watanzania kushiriki katika michezo baada ya shughuli zao
katika suala zima la kujenga Afya zao na kuleta burudani hakika taswira hiyo
itajenga taifa la watu wenye Afya na kuondoa magonjwa mbalimbali
yanayoinyemelea jamii yetu.
Timu
zilizoshiriki katika bonanza hilo ni pamoja na Arusha Coaches,kampuni ya
Benson,Mango Garden ambao walikuwa wageni waalikwa kutoka jijini Dar es salaam
na wenyeji Timu ya Kitambi Noma zote za
jijini Arusha ambapo katika soka timu zote zilicheza kwa mzunguko na
kujikusanyia pointi na bingwa kupatikana.
Katika mechi
ya kwanza kati ya Arusha coaches walifungwa bao moja bila majibu na timu ya
mango garden ikifuatiwa na mechi ya wenyeji kitambi noma na timu ya bensons na
kujikuta benson wakipigiliwa kwa bao mbili bila majibu mechi iliyofuata ni kati
ya timu ya makocha wa mkoa wa Arusha na
Benson mchezo ulioisha kwa Arusha Coaches kuwapigilia bila huruma benson kwa
bao 3 bila majibu.
Kwenye
mchezo wa kuvuta kamba timu ya kitambi noma iliibuka mshindi katika fainali
yake na timu ya benson huku benson na kitambi noma wakiibuka washindi kwa
kugawana kuku moja moja katika mashindano ya kukimbiza kuku huku bonanza hilo
likifana na kuwapa burudani murua wakazi wa jiji hili na viunga wake.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia