Naibu
Meya wa Jiji la Arusha, Prosper Msofe (kushoto) ambaye pia ni Diwani wa
Kata ya Daraja Mbili kupitia CHADEMA na Diwani wa Kata ya Levolosi,
Ephata Nanyaro nae kupitia Chadema, wakisubiri kupata matibabu baada ya
kupata kipigo kutoka kwa mgambo wa Jiji la Arusha leo wakati wakiwatetea
Wamachinga.
Kwa mujibu wa Diwani Nanyaro, anasimulia kwamba leo asubuhi alipata taarifa kuwa mgambo wa Jiji wanawapiga wananchi wafanyabiashara ndogondogo na kupora mali zao maeneo ya Kata yake, ndipo akaelekea kukutana na Naibu Meya kujionea hali halisi. Anasema alipofika alijaribu kuwasihi mgambo hao kuwa sio utaratibu kuwapiga wananchi maana hata taratibu za ukamataji haziruhusu kupiga raia.
Nanyaro anasema wakiwa wanawashauri mgambo hao, ghafla walishangaa na yeye amezingirwa na kuanza kupigwa sambamba na Msofe huku mgambo hao wakiwaeleza Madiwani hao kuwa wamekuwa na kiherehere sana.

Naibu Meya anenaAkizungumza
na Blog hii Mh. Naibu Meya Prosper Msoffe ameeleza kiini cha tatizo
kuwa yeye kama kiongozi wa wananchi amekuwa akipokea malalamiko mengi ya
wananchi kupigwa, wengine kuvunjwa miguu, mali kuporwa na mgambo, mali
kifadhiwa depoti hadi kuoza. Hivyo akaamua kufika eneo la depoti leo
kujionea hali halisi na kuzungumza na mgambo na wananchi, baada ya
kufika eneo la tukio alianza kushambuliwa kwa virungu na mateke, huku
wakisema wewe umekuwa kiherehere sana na mtetezi wa wananchi sasa
tunakukomesha.
Mh. Naibu Meya alishangazwa pia kuona kiongozi
mwenzake Diwani wa Levolosi kufika pale nae akapigwa, na kuhoji kama
yeye Naibu Meya amepigwa, hali ikoje kwa wananchi wa kawaida!??
Hatua za kisheria dhidi ya mgambo hao
Hadi
tunaandika taarifa hii, Madiwani hao walikuwa wanaandaa utaratibu wa
kushughulikia swala hilo wakidai kwamba mgambo hao wameonesha utovu
mkubwa wa nidhamu na ukiukwaji wa sheria kwa kuwapiga waajiri wao.
Msofe na Nayaro wamelaani vikali tukio hilo na kuahidi kufuatilia ili
sheria ichukue mkondo wake na iwe fundisho wa wengine.
Kadi ya matibabu ya Kituo cha Afya Levolosi, ikionyesha Mh. Naibu Meya ALIVYOUMIZWA
Wananchi
na Wanachama wa Chadema Wakiwa nje ya Geti la depoti ya Jiji na Kituo
cha Afya cha Levolosi wakisubiri hatma ya Viongozi wao.
Diwani
Nanyaro na Naibu Meya Msofe wakimweleza Mwandishi Filbert Rweyemamu
hali ilivyokuwa hadi kupigwa kwa kile walichodai kutetea wananchi
wanyonge dhidi ya uonevu, ukatili na ukandamizaji unaofanywa na askari
wa Jiji.
‘Siamini kama Wafanyakazi wangu wanaweza nishambulia kiasi hiki’ Maneno ya Nanyaro akikagua ripoti ya dakatari
Mh Kessy, Diwani wa Kaloleni (anayeongea na simu) alipofika Hospitalini hapo kuwajulia hali viongozi wenzake.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia