Ticker

6/recent/ticker-posts

BUNUELIA BRYTON NDIE MSHINDI WA MBIO ZA HISANI UJUMBE DHIDI YA UGONJWA WA KISUKARI


Banuelia ameshinda mbio hizo upande wa wanawake akikimbia kwa dakika 31:18:53, nafasi ya pili ikaenda kwa mwanariadha chipukizi, Rose Kasusura, mwenye umri wa miaka 14, kutoka katika klabu ya michezo ya Kibo, ambaye alitumia dakika 45:13:52.

Nafasi ya tatu ya mtifuano huo ulioteka hisia za wengi ilikwenda kwa Teresia Kasim aliyetumia muda wa dakika 54:59:53.

Katika mbio za wanaume kilomita 8, mshindi alikuwa ni Marcel Ntandu wa TPC, ambaye alitumia dakika 24:59:41, nafasi ya pili ikienda kwa Matayo Milau wa Kili Athletic, aliyekimbia kwa dakika 25:01:37 na nafasi ya tatu ikienda kwa Paulo Bajuta (dakika 25:32:80).

Akizungmza baada ya kushinda mbio hizo, Banuelia ambaye ni bingwa wa taifa katika mbio za nyika, alisema kuwa ameamua kujipumzisha na mashindano makubwa, lakini anatumia mashindano madogo madogo kama hayo kujiweka sawa kabla ya kurudi upya katika mbio.

Alisema kwa muda mrefu amekuwa kimya, hivyo sio sahihi kurudi uwanjani na anachokifanya hivi sasa ni kuhakikisha anarejea makali yake, huku akiahidi kuwa hivi karibuni watu wamtarajie Banuelia waliyekuwa wamemzoea.

Kwa upande wake, Meneja Msaidizi wa Benki ya Akiba (ACB), Tawi la Moshi, Damari Kanyama, alisema lengo la kudhamini mbio hizo ni kutokana na kutambua umuhimu wa michezo katika afya ya binadamu na kuongeza kuwa hiyo ndiyo njia pekee ya kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari.

Naye Muuguzi wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Benedeth Ollomi, alisema wameamua kushiriki mbio hizo kama sehemu ya mpango wao wa afya kupitia michezo na mazoezi na kuongeza kuwa KCMC imejipanga kuhakikisha wanatumia michezo kuhamasisha kampeni dhidi ya kisukari ambayo imaenza kushika kasi mkoani Kilimanjaro.

Mbio hizo zimeratibiwa na klabu ya michezo ya Kibo na kudhamniniwa na KCMC, Japhary Dispensary, Zumba land, ACB, Central Palace, Honest Block Reboring nk, ambapo washindi walikabidhiwa viatu vya kukimbilia na vyeti.

Post a Comment

0 Comments