Jengo
linalotumika kwa makazi ya walemavu huko Rasibura, katika Mji wa Lindi
likiwa katika hali mbaya ya uchakavu. Jengo hilo awali lilikuwa
likitumiwa kama gereza na Jeshi la Magereza la Lindi na baadaye
kukabidhiwa kwa Idara ya Ustawi wa Jamii na ndipo walipoamua kutumia
kama jengo la kuwatunzia watu wenye ulemavu.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akitembelea sehemu mbalimbali za jengo la
kuwatunzia walemavu huko Rasibura Mjini Lindi akiongozwa na Mlezi wa
Kituo hicho Ndugu Simon Mnimbo kutoka Kanisa Katoliki Jimbo la Lindi
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akitembelea sehemu mbalimbali za jengo la
kuwatunzia walemavu huko Rasibura Mjini Lindi akiongozwa na Mlezi wa
Kituo hicho Ndugu Simon Mnimbo kutoka Kanisa Katoliki Jimbo la Lindi
Mke
wa Rais, Mama Salma Kikwete akiongea na watu wenye ulemavu mbalimbali
wanaoishi Rasibura baada ya kutembelea sehemu mbalimali za jengo lao.
Mama Salma aliwatembelea walemavu hao wakati wa sikukuu ya pasaka na
kuwapa zawadi mbalimbali za sikukuu hiyo
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na mtoto Idd Mohamed Chitawala
ambaye ni mlemavu wa macho anayeishi katika kituo cha rasibura pamoja na
Baba yake Mzazi Bwana Mohamed Chitawala.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi Kiongozi wa Kituo cha walemavu
cha Raisbura Bwana Mohamed Chitawala baadhi ya vyakula alivyowaletea-
mchele, unga, mafuta ya kupikia, sukai, soda na vinginevyo wakati
alipotembelea kituo cha walemavu cha Rasibura huko Lindi siku ya Pasaka
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi zawadi yake ya Pasaka Ndugu
Theresia Thomas ambaye ni mlemavu wa viungo anayeishi katika kituo cha
Rasibura huko Lindi. Baadaye Mama Salma anaonekana akipiga picha naye
akiwa amelala kitandani kwani Theresia hawezi kukaa wala kusimama.
Baadaye Mama Salma anaonekana akipiga picha naye akiwa amelala kitandani kwani Theresia hawezi kukaa wala kusimama
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na baadhi ya watu wenye ulemavu
wanaoishi katika Kituo cha Rasibura mara baada ya kuwakabidhi zawadi zao
za Pasaka. Picha na John Lukuwi