Tangazo
la onesho la Documentary : Tanzania; a Journey within, kama linavyoneka
siku ya ufunguzi wake hapo April 25 jiji New York , siku ambayo Jumuiya
ya Kimataifa ilikuwa ikiadhimisha siku ya Malaria Duniani. Kwa mujibu
wa waandaji wa Documetary hiyo ambayo wahusika wake wakuu ni dada wa
Kimarekani Kristen Kenney na kaka wa kitanzania, Venance Ndibalema
mapato yatokanayo na onesho la decumentary hiyo yanapelekwa kusaidia
mapambano dhidi ya ugonjwa malaria nchi Tanzania.
washiriki
wa onyesho wakiwa wamenyayua pipi kijiti ambazo ujumbe wake ulikuwa
"Malaria Sucks" ikiwa ni ishara yao ya kuunga mkono mapambano dhidi ya
Malaria.
Washiriki
wengi walijitokeza kuangalia documentatry hiyo ambayo tayari
imeshajizoelea sifa tele, washiriki wengi licha ya kuvutiwa ma maudhui
yake baadhi yao walijikuta wakitoa machozi baada ya kuguswa na
walichokiona
Wahusika
wakuu wa Documentary ambayo imetayarishwa nchini Tanzania, wakijiandaa
kujibu maswali, kutoka kushoto, Kristen Kennye, Venance Ndibalema na Bi,
Sylvia Caminer ambaye ndiye aliyeongaza decumentary hiyo, Sylvia ni
mshindi wa Tuzo kadhaa za Emmy.