BREAKING NEWS

Friday, April 25, 2014

WAFUGAJI,WAUZA DAWA ZA MIFUGO WAFUNDWA



ZAIDI ya wafugaji 300 na wafanyabiashara wa maduka ya dawa za kilimo na mifugo, wamepatiwa mafunzo ya utumiaji dawa za kutibu mifugo ya aina mbalimbali na virutubisho vinavyotolewa na Kampuni ya BYTRADE (T) Ltd.
Akizungumza katika semina ya kuwajengea uwezo wafugaji na wauza dawa za mifugo, Mkuu wa Idara ya Wanyama wa kampuni hiyo, Dk. Omary Magoma, alisema mifugo yote inasumbuliwa na maradhi mbalimbali, hivyo inahitaji dawa za kuikinga na kuitibu.
Magoma pia aliwataka wafugaji wanapoona wanyama wao wanadhohofika waache kuwapa dawa bila ya kugundua aina ya ugonjwa na kuwashauri kutumia bidhaa za kampuni hiyo kwani ndiyo suluhu ya magonjwa na virutubisho kwa wanyama na mimea.
“Kwa mfano dawa hii ya GUT-O-CID ni dawa ya kudhibiti kwa ufanisi bakteria waenezao magonjwa sumbufu kama Salmonella, E.coli. Pia inadhibiti uzalishwaji wa gesi ya Ammonia inayosababisha harufu kali bandani ambayo ni chazo cha mafua kwa wanyama, hasa kuku na nguruwe,” alisema Dk. Magoma.
Alisema kuwa dawa hiyo ambayo huchanganywa kwenye chakula, hukilinda dhidi ya maambukizi ya bakteria na fangasi, pia huongeza ladha ya chakula na kuongeza kuwa kwa sasa wameingiza dawa aina 11 sokoni.
Alizitaja baadhi ya dawa hizo kuwa ni Mult-Aminovet ambayo ina aina zote za vitamin na Amino Acid huku akibainisha kwamba madini yanaweza kufidia upungufu katika vyakula vya wanyama na kuboresha kiwango cha utagaji na ubora wa mayai.
Alisema inaongeza matokeo bora kwa ng’ombe wa maziwa na hutumika kuondoa msongo wakati wa matibabu chanjo, joto kali na usafirishaji kwa kuku huku pia akiitaja dawa aina ya Enziver kuwa inaboresha uyeyushwaji na unyonywaji wa chakula mwilini mwa wanyama na hurahisisha pia ukuaji kwa kuku na nguruwe.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates