Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya UNHWA ya Jamhuri ya Korea Kusini Bw. Young Woo Jin na ujumbe wake na uongozi wa NIMR walipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo |
Mkurugenzi Mkuu wa NIMR Dk. Mwele Malecela.
Taasisi ya taifa ya utafiti wa
magonjwa ya binadamu Tanzania (NIMR), imesaini mkataba wa ushirikiano na kampuni ya
UNHWA ya Jamhuri ya Korea Kusini ambapo kampuni hiyo itaisaidia NIMR teknolojia mpya
ya kufanya ugunduzi wa dawa za binadamu kwa kutumia mimea.
Makubaliano hayo yamesainiwa
jijini Dar es salaam pembezoni mwa kongamano la 28 la kisayansi la NIMR, ambapo
mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo Dk. Mwele Malecela amesema hatua hiyo ni muhimu
katika shughuli za utafiti wa afya nchini na maendeleo ya taasisi kwa ujumla.
Dk. Mwele amesema teknolojia
hiyo itaongeza uwezo wa kiwanda cha taasisi cha kutengeneza dawa kwa kutumia
mimea kilichopo eneo la Mabibo External jijini Dar es salaam na kwamba
itawezesha taasisi kujikita zaidi katika utengenezaji wa dawa za saratani
mbalimbali pamoja na za kusaidia udhibiti wa virusi vya ukimwi.
Kwa upande wake afisa mtendaji
mkuu wa kampuni hiyo ya NHWA bw. YOUNG WOO JIN amesema kampuni yake imefikia
hatua hiyo kutokana na mchango wa NIMR katika masuala ya tafiti na ugunduzi wa
dawa ambapo ameahidi kuendelea kushirikiana na taasisi hiyo katika kiteknolojia
ili kuiongezea uwezo.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia