wanenguaji wa bendi ya mashujaa
BENDI
mpya inayotamba kwa sasa hapa nchini na ambayo imechukuwa tuzo
mbalimbali za muziki hapa nchini (MASHUJAA BAND) JUMAPILI april 20
inatarajia kushuka jijini Arusha katika ukumbi wa Triple A kuwapa
burudani wakazi wa jiji hilo na vitongoji vyake.
Akiongea
na waandishi wa habari muandaaji wa onyesho hilo kutoka katika kampuni
ya Rickenet Intertament Papa Ernest alisema kuwa bendi hii ya mashujaa
itatua jijini hapa kwa ajili ya onyesho hilo ambapo alilifafanua kuwa
tangu bendi hii kuanzishwa hii ni onyesho lao la kwanza kufanya jijini
hapa.
Alisema
kuwa bendi nzima ya mashujaa inatarajiwa kutia timu jijini hapa wakiwa
na wanamuziki wake wote ambapo aliwataja baadhi ya wanamuziki wa bendi
hiyo kuwa ni pamoja na Chaz Baba,
Alifafanu
kuwa bendi hii imedhamiria ‘kufunika’ katika onyesho hilo na
wamejipanga kufunika bendi zote ambazo zimeshawahi kufanya onyesho
katika jiji hili la Arusha kwani bendi hii ina historia nzuri katika
muziki wa Tanzania haswa katika maonyesho yao mbalimbali ambayo
wameshayafanya hapanchini.
muandaaji wa onyesho la mashujaa kampuni
ya Rickenet Intertament Papa Ernest
Aidha
Ernest alisema kuwa ameamua kuwaletea wakazi hawa wa jiji la Arusha
bendi hii kwani bendi hii imekuwa inafanya vyema katika tasinia hii ya
muziki wa dansi ambapo alifafanua kuwa kwa mwaka huu bendi hii ya
mashujaa inashikilia tuzo tano za muziki hapa nchini.
Alitaja
kiingilio cha shindano hili ni shilingi10000 kwa kila mmoja huku
akiwasihi wakazi wa mkoa wa Arusha kujitokeza kwa wingi kuangalia bendi
hii ambayo inawanamuziki wengi ambao wanajua kutawala jukwa a kwa kuimba
pamoja na kucheza.