
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa Kapalamsenga wilayani Mpanda mkoani Katavi.

Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa
Kapalamsenga ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa CCM inazidi kuimarika
na kuzidi kuaminika kwa wananchi siku hadi siku .

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungmza mbele ya waandishi wa
habari kwenye eneo lililopaswa kujengwa bandari ya Karema baada ya
kujionea mradi wa ujenzi wa bandari ya Karema ulivyosimama.

Katibu
Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia majengo yaliyokuwa yameenza
kujengwa kisha mradi wa ujenzi wa bandari kusimama kwa muda mrefu,Katibu
Mkuu yupo kwenye ziara ya siku tatu mkoani Katavi ambapo moja ya
shughuli atakazofanya ni kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na
kujenga na kuimarisha Chama.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,akiongozana na Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye , Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dk. Rajab
Rutengwe wakikagua mradi wa Ujenzi wa Mwalo uliopo kijiji cha Ikola.
- Awaomba radhi wananchi wa Karema kwa kuchelewa kukamilika kwa mradi wa bandari ambao umesimama kabisa baada ya mkandarasi aliyepewa mradi huo kushindwa kuumaliza .
- Asikitishwa na watumishi wengi wa serikali kuendeleza tabia ya umangi meza kwani miradi mingine inasimama kwa kipindi kirefu kwa sababu kuna kiongozi wa serikali amechelewa kujibu barua itakayofanikisha mradi kuendelea na kumalizika kwa wakati.
- Asisitiza Viongozi na wana CCM kuwa wakali katika kusimamia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na kusema si vyema tusubiri wapinzani waseme ,tunayaona matatizo inabidi wana CCM wayasemee wenyewe na si vinginevyo.