Timu ya Taifa
ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania imetwaa ubingwa wa Dunia wa Watoto wa Mitaani
baada ya jana (Aprili 6 mwaka huu) kuilaza Burundi mabao 3-1 katika mchezo wa fainali
uliochezwa jijini Rio de Janeiro, Brazil.
Mshambuliaji
Frank William alifunga mabao matatu katika mechi hiyo iliyochezwa uwanja
mkongwe na maarufu wa klabu ya Fluminense huku mgeni rasmi akiwa Waziri wa
Fedha wa Uingereza, George Osborne.
Tanzania
ilipata tiketi ya kucheza fainali baada ya kuitandika Marekani mabao 6-1 ambapo
hadi mapumziko ilikuwa mbele kwa mabao 4-0.
Burundi
ilipata tiketi ya kucheza fainali baada ya kuifunga Pakistan mabao 4-3 katika mechi
ya nusu fainali ya pili.
Aidha katika mchezo wa ufunguzi uliozikutanisha Tanzania na Burundi na kutoka sare ya goli 2-2.
Timu ya
Tanzania inarejea nchini Alhamisi (Aprili 10 mwaka huu) ambapo itatua Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 10 jioni kwa ndege ya Emirates.