Katika
kile kinachoonekana kuwa mfululizo wa matukio ya ulipukaji wa mabomu
Jijini Arusha, jioni ya jana Aprili 13, 2014 ulitokea mlipuko wa
kinachodhaniwa kuwa bomu la kurushwa kwa mkono katika Bar maarufu kwa
maonesho ya mechi za mpira wa Ulaya, ijulikananyo kama Arusha Night Park
aka M.T.K Bar iliyopo maeneo ya Mianzini na kujeruhi zaidi ya watu 20
wengi wao wakiwa wateja waliojazana kushuhudia mpambano baina ya Chelsea
na Swansea City za Englanda majira ya saa moja na nusu jioni.
Majeruhi
walikimbizwa hospitali za Mt Meru na Dr Mohamed kwa matibabu ya haraka,
na hakuna taarifa rasmi ya mtu aliyepoteza maisha ingawa baadhi ya
walionusurika wanshuhudia kuwepo watu waliokatika miguu.
Taarifa ya awali kutoka Jeshi la Polisi inaeleza kuwa bomu hilo ni la kutengenezwa kienyeji baada ya kukuta vipande vya vyuma na misum

Majeruhi walikimbizwa hospitali za Mt Meru na Dr Mohamed kwa matibabu
ya haraka, na hakuna taarifa rasmi ya mtu aliyepoteza maisha ingawa
baadhi ya walionusurika wanshuhudia kuwepo watu waliokatika miguu.
Taarifa ya awali kutoka Jeshi la Polisi inaeleza kuwa bomu hilo ni la kutengenezwa kienyeji baada ya kukuta vipande vya vyuma na misumari eneo la mlipuko. Aidha taarifa zaidi zinaeleza kuwa bomu hilo lilirushwa na mtu anayeendelea kusakwa na Jeshi la Polisi likiwa kwenye mfuko wa plastiki kuelekea katikati ya mashabiki hao.
Bado haijaweza kufahamika sababu hasa za zilizopelekea mlipuko huo ingawa kuna watu wenye hisia tofauti, baadhi wakidhani ni maswala ya ushindani wa kibiashara na wengine wakihisi huenda ni maswala ya kisiasa ama utalii.
Pamoja na hayo, Mkuu wa Mkoa Mh Magessa Mulongo amewataka wakazi wa Arusha kuwa watulivu katika kipindi hiki wakisubiri taarifa rasmi ya kilichotokea na kuahidi kuwa Jeshi la Polisi litafanya uchunguzi na kubaini wahusika.
tukio hili limetokea wakati Jiji hili bado lina kumbukumbu ya matukio mengine ya mshambulizi ya bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi lililopo Olasiti na shambulio lingine katika mkutano wa Chadema uwanja wa Soweto wakifunga kampeni za udiwani Juni 15, 2013, ambapo takribani watu sita waliuwawa na zaidi ya 100 kujeruhiwa vibaya huku baadhi wakipoteza viuongo.

Sehemu ambayo ndipo bomu hilo lililipuka na kusambaa ikiwa imeanza kufanyiwa uchunguzi na wataalamu wa mabomu. 

Baadhi ya wananchi waliofika eneo la mlipuko kutaka kujua na kushuhudia kilichojiri

Picha hizi tatu juu japo ni hafifu lakini zinaweza kuonesha baadhi ya majeruhi wa mlipuko huo, kwa hisani ya mdau Chris Nnko