Oparesheni Kamata Bodaboda na Bajaji ikiwa inaendelea upande wa Mwenge mataa ambapo Bajaji nyingi zimekamatwa
Askari
wa Usalama wa Barabarani akiwa anawaandikisha Baadhi ya Bodaboda na
Bajaji wenye makosa mbalimbali ili waweze kulipia tozo pamoja na
kupelekwa kituo cha Polisi.
Baadhi ya Bodaboda na Bajaji wakiwa wanangojea Hatma yao baada ya kukamatwa
Huu ni upande wa kutokea Mwenge kuelekea Posta ambapo Bajaji haziruhusiwi kuvuka hapo kuelekea Posta
Baadhi ya Madereva wa Bajaji na Boda boda wakijadiliana Juu ya swala hilo la kuzuiliwa kuelekea Posta
Baadhi ya Bodaboda zikiwa zimekamatwa
Madereva wa Boda Boda na Bajaji wakipata maelezo ya kina ya kwanini wamezuiliwa kwenda Posta wakitokea Mwenge
Mmoja
wa Madereva wa Bodaboda akiwa amekaa kwa Mawazo asijue anafanya nini
Baada ya Bodaboda yake kukamatwa na Kupelekwa Polisi.
Oparesheni
Nzito ya kuzuia Bodaboda na Bajaji zisifanye safari zake kutoka Mwenge
na maeneo mengine kuelekea mjini Posta imechukua sura mpya leo baada ya
Askari wa Usalama wa Barabarani kuanza kukamata Bodaboda na Bajaji zote
zinazovuka Mwenge kuelekea Posta, Zoezi hilo ambalo limefanyika Mwenge
Mataa Jijini Dar limeendelea kufanyika na kufamikiwa kuwanasa wengi.
Kwa
mujibu wa Msemaji na Muongozaji wa Oparesheni hiyo ambaye hakutaka
kutajwa jina lake alisema kwamba wameamua kufanya hivyo ili kuzuia
Msongamano wa Magari pamoja na bodaboda pia Bajaji kuelekea Mjini Posta,
Aliongeza kuwa kumekuwa na uhalifu sana wa Silaha unaotumiwa na
bodaboda hasa maeneo ya mjini hivyo ndio maana wameamua kuzuia.
"Tumefanya
hivi ili kuepusha msongamano kuelekea Posta, lakini pia kumekuwa na
uhalifu sana unaotumiwa kwa njia ya Bodaboda hivyo tunafanya oparesheni
hii ili kupunguza tatizo hili. Tulicho kifanya tumewaruhusu kufanya
safari pembezoni mwa mji tuu hivyo Eneo la Mwenge kwa sasa Limeingia
katika zone ya eneo la Mjini,Kama tuliweza kuzuia Daladala ndogo"Hiace"
pia na hawa watakuja kuelewa ingawa ni zoezi gumu na linalo hitaji elimu
ya ziada ambayo tumesha anza kuwapa na tunaendelea kuwapa" alimalizia
kwa kusema "Pia hii ni Oparesheni ya kawaida tuu ya kukamata wale ambao
hawana Leseni za kuendesha vyombo hivi pamoja na makosa mbalimbali"
alisema Polisi huyo.
Kwa
mujibu wa madereva wa Bodaboda na Bajaji wamesema kwamba huo ni uonevu
kuwakataza wao wasiweze kwenda Mjini kwani na wao wanatafuta ridhiki yao
na wameomba Serikali iwasaidie wapatiwe njia mbadala ya wao kwenda
maeneo hayo.
Wanao
ruhusiwa kwenda Posta na Bajaji au Bodaboda ni wale ambao ni wamiliki
binafsi na wanatakiwa wapite njia hizo wakiwa Bila abiria yoyote.