Kikundi
cha ngoma toka Jeshi la Kujenga Taifa kikitumbuiza kwenye uzinduzi wa
maonyesho ya miaka 50 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi mmoja
Mgeni
Rasmi wa maonyesho ya miaka 50 ya Muungano ,Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Seif Sharif Hamad akitoa hutuba ya
ufunguzi wa maonyesho hayo katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es
Salaam.
Chungu
na kibuyu vilivyotumika na waasisi wa Muungano kuchanganya udongo mwaka
1964, vinapatikana katika banda la Ofisi ya Makamu wa Rais.
Mgeni
Rasmi wa maonyesho ya miaka 50 ya Muungano ,Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Seif Sharif Hamad akiwa ndani ya Banda
la Ofisi ya Makamu wa Rais akipata maelekezo juu ya chungu na vibuyu
vilivyotumika kuchanganya udongo wakati wa Muungano wa Tanganyika na
Zanziabr mwaka 1964
Wananchi
mbalimbali waliojitokeza kutemebelea banda la Ofisi ya Makamu wa Rais
wakiangalia majarida mbalimbali bandani hapo na kusaini kitabu cha
wageni.