Mkuu wa Bandari ya Mtwara, Absalom Bohela
(kushoto) akikabidhi msaada wa madawati 110 yenye thamani ya shilingi milioni
20 kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh. Ludovick Mwananzila (kulia) wakati wa hafla
ya makabidhiano iliyofanyika hivi karibuni katika kijiji cha Mahumbika
kilichopo Lindi vijijini.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh. Ludovick Mwananzila (kulia) na
Mkuu wa Bandari ya Mtwara, Absalom
Bohela (kushoto) wakiwa na baadhi ya wanafunzi wa shule ya
msingi Mahumbika wakati wa kukabidhi msaada wa madawati 110 yenye thamani ya
shilingi milioni 20 kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kwa
shule za mkoa wa Lindi hivi karibuni.