Kutoka
kushoto: Wasanii Dk. Cheni, Bi. Mwenda, Profesa Jay na Wema Sepetu
wakishiriki kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa GlobaL TV Online
jana.
Wema Sepetu na Profesa Jay wakifunua vitambaa wakati wa uzinduzi wa GlobaL TV Online jana katika ofisi za Global Publishers Ltd.
GlobaL TV Online baada ya kuzinduliwa rasmi.
Mkurugenzi
wa Global Publishers & General Enterprises Ltd, Eric Shigongo
pamoja na staa wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu wakikata keki wakati wa
uzinduzi huo.
Mkongwe wa sanaa ya maigizo Bongo, Fatuma Makongoro 'Bi. Mwenda' akijiandaa kufungua shampeini.
Shampeini zikiwa tayari kufunguliwa.
....
IT'S CHEERS TIME...
Waalikwa na wafanyakazi wa Global wakigonga 'Cheers'.
Prof Jay, Bi. Mwenda na Steve Nyerere wakigonga 'cheers'.
Shigongo
akigonga 'cheers' na Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Richard
Manyota (kulia) na Oscar Ndauka ambaye ni Mhariri Kiongozi Magazeti
Pendwa (katikati).
Mastaa wakigonga cheers.
...Cheers.
Kampuni
ya Global Publishers & General Enterprises Ltd, wachapishaji wa
Magazeti ya Uwazi, Championi, Amani, Risasi, Ijumaa na Ijumaa Wikienda
jana ilizindua Global TV Online ambayo ni televisheni inayoruka
mtandaoni kupitia tovuti ya kampuni hiyo ya www.globalpublishers.info
ndani ya ofisi zake zilizopo Mwenge-Bamaga jijini Dar es Salaam. Katika
uzinduzi huo, mastaa kibao walihudhuria na kupata fursa ya kuona baadhi
ya vipindi kutoka Global TV Online pamoja na kutoa maoni yao kuhusu
uboreshwaji wa TV hiyo. Mbali na tukio hilo, mastaa waliongoza zoezi la
kukata utepe, kufungua shampeini na kukata keki kuashiria uzinduzi rasmi
wa Global TV Online.