Mkurugenzi
wa upelelezi wa makosa ya jinai cp Issaya Mngulu akiongea na
waandishi wa habari hivi leo amesema kuwa mlipuko uliotokea juzi katika
bar ya Arusha Night park(Matako bar) ulikuwa ni wabomu la kutengenezwa
kienyeji
Amesema
kuwa katika tukio hilo la bomu watu kumi na tano walijeruliwa na
walifikishwa katika hospitali ya mkoa ya Mounti meru lakini mpaka sasa
watu wat u saba wameruhusiwa na wengine nane bado wamelazwa katika
hospita hiyo hiyo ya mkoa
Aidha
ameongeza kuwa jeshi la polisi limekamata kitu ambacho kinasadikiwa
ni kifaa cha kutengenezea bomu ambacho kimekutwa kimetelekezwa katika
bar moja inayojulikana kama washngton bar ilipo jijini hapa.