Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
Mhe Saidi Meck Sadiki baada ya kuwasili jana April 4, 2014 katika uwanja
wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea Brussels, Ubelgiji,
alikofanya ziara ya kikazi ya siku mbili na kuhudhuria mkutano wa
mataifa ya Afrika na nchi za Jumuiya ya Ulaya. Kabla ya hapo Rais
Kikwete alifanya zaiara ya kiserikali ya siku tatu nchini Uingereza kwa
mwaliko wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Mhe David Camaron. PICHA NA IKULU